Welbeck ndiyo basi tena Arsenal

Muktasari:

  • Kocha wa Arsenal, Unai Emery alisema mchezaji huyo amefanyiwa upasuaji wa pili katika mguu wa kulia uliovunjika Alhamisi iliyopita katika mchezo wa Kombe la Europa dhidi ya Sporting Lisbon ya Ureno.

London, England. Danny Welbeck amepata pigo baada ya kuumia vibaya kifundo cha mguu.

Kocha wa Arsenal, Unai Emery alisema mchezaji huyo amefanyiwa upasuaji wa pili katika mguu wa kulia uliovunjika Alhamisi iliyopita katika mchezo wa Kombe la Europa dhidi ya Sporting Lisbon ya Ureno.

“Imebainika Welbeck aliumia kifundo cha mguu, amelazimika kufanyiwa upasuaji wa pili kutibu jeraha, atakuwa nje kwa zaidi ya miezi mitano na hatutarajii kumtumia msimu huu,” alisema Emery.

Welbeck, ambaye ameifungia Arsenal mabao matano msimu huu, aliitwa katika kikosi cha England kinachojiandaa na mechi za wiki ijayo dhidi ya Marekani na Croatia.