Wazee wa Kupapasa wawasogeza mkiani Mwadui FC

Muktasari:

  • Kikosi cha Mwadui FC kimeendelea kukaa mkiani kwenye michuano ya Ligi Kuu Bara baada ya kutoka suluhu na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga.

Dar es Salaam. Mwadui FC imeshindwa kuwatambia Wazee wa Kupapasa kikosi cha Ruvu Shooting baada ya kumaliza kwa suluhu katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga.
Mwadui ambao suluhu ya mchezo huo, imewasogeza nafasi mbili kutoka mkiani walipokuwa katika msimamo wa Ligi Kuu Bara yenye timu 20, wakiwa na pointi sita.
Kikosi hicho kilicho kwenye machimbo ya Almasi, Walipambana kwa nguvu kuhakikisha wanapata bao lakini washambuliaji wao waliochezeshwa na kiungo, Abdallah Seseme walishindwa kumalizia.   
Kutokana na matokeo hayo, Ruvu Shooting wao wamepanda mpaka nafasi ya 12, na pointi 10.
NDANDA NA MBEYA CITY
Katika mchezo mwingine kati ya Ndanda FC na Mbeya City zimemaliza kwa suluhu kwenye mechi iliyopigwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
Mechi zote hizo ni za raundi ya 10, kwenye Ligi Kuu Bara ambayo mpaka sasa bado haijapata Mdhamini Mkuu.
Kwa matokeo hayo, Mbeya City nayo imepanda mpaka nafasi ya nane na pointi 14, wakati Ndanda inabaki nafasi ya 15 na pointi tisa.