Wawa, Zana wapewa neno

Muktasari:

  • Mechi za mikoani kwa Simba na Yanga sio zakuzichukilia poa wanatakiwa kujipanga kisawasawa kama anavyozungumza Jocab Masawe wa Stand United 'Chama la Wana' aliyewaliza Wanajangwani msimu huu.

Dar es Salaam. YANGA imempa kiburi straika wa Stand United, Jacob Masawe ambae aliwafunga Uwanja wa Kambarage, Shinyanga ametunisha misuri dhidi ya mabeki wa Simba, Pascal Wawa na Zana Oumar Coulibaly kwamba hajaona maajabu yao na kama wanabisha wamuulize Kelvin Yondan.

Masawe aliliambia Mwanaspoti kwamba kinachowatofautisha na Simba na Yanga ni uchumi na ukongwe ambao umefanya wawe na mashabiki wa kutosha lakini kiuwezo hajaona cha kumshangaza.

Alipoulizwa anawaonaje Wawa na Zana na anadhani watakuwa na changamoto gani kwenye mechi yao ya kesho Jumapili! Masawe alijibu kuwa "Hivi kuna beki anayesifika kama Yondan wa Yanga ubora na vitimbwi vyake!lakini muulize kilimkuta nini kwenye dimba letu la Kambarage.

"Kifupi siwezi kuwadharau na pia kuwaogopa kupitia wao nitawafurahisha mashabiki wangu kwa kuandika rekodi nyingine baada ya kuwafunga Yanga inawezekana na wala sio miujiza.

"Zamani tulikuwa tukisikia majina ya wachezaji wa Simba na Yanga kabla ya kuingia uwanjani unaweza ukaghairi lakini kwa sasa naona kawaida isipokuwa majina yao yanakuzwa na mashabiki wa