Wawa, Kotei, Zana wajipanga upya kuivaa TP Mazembe kwao

Muktasari:

 

  • Mechi hii ya nyumbani ilikuwa muhimu kwetu kupata matokeo ya ushindi kama ilivyokuwa katika mechi zote ambazo tumecheza nyumbani msimu huu katika mshindano haya ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Dar es Salaam. Wachezaji wa Simba mbali ya kushindwa kupata ushindi katika mechi ya kwanza na TP Mazembe wanaamini wanakwenda kujipanga na kupata matokeo mazuri katika mechi ya marudiano itakayochezwa Aprili 13, pale DR Congo.

Pascal Wawa alisema kwanza niliona kama nimeiangusha timu baada ya kuumia kwani mchango wangu ulikuwa unahitajika ili tuweze kupambana kwa pamoja na wachezaji wenzangu kufikia malengo ambayo tumejipangia lakini nilishindwa kuendelea kutokana nilikuwa nasikia maumivu makali sana.

Wawa alisema mechi na marudiano Lubumbashi itakuwa ngumu kuliko mechi ya kwanza waliocheza nyumbani, lakini anawaamini wachezaji wanzake wanauwezo wa kwenda kupambana na kupata matokeo ambayo watakuwa wanayahitaji.

"Mechi ilikuwa nzuri kwetu na tulipata nafasi si chini ya mbili za kufunga lakini tulishindwa kufanya hivyo   geza kwa upande wetu kulingana na wapinzani walivyo ili kuwa kama silaha na kufanya vizuri mchezo wa mwisho," alisema.

"Mwisho nisiache kuwapongeza mashabiki wa Simba wote waliojitokeza katika mechi ya hapa nyumbani kwani vile ambavyo wanajisikia wao hata wachezaji ni hivyo hivyo nawahidi tupo pamoja na tutaendelea kushindana zaidi yao," alisema Wawa.

Zana Coulibaly alisema wachezaji wote tuliingia na kiu kubwa ya kufanya vizuri na ndio maana tulikuwa tunapambana muda wote lakini bahati mbaya ilikuwa kwetu kwa kushindwa kutumia nafasi za kufunga ambazo tulikuwa temetengeneza.

Coulibaly alisema tunaelekeza nguvu katika mchezo wa marudiano makosa ambayo tuliyafanya katika mchezo huu makocha wetu wameyaona na watakwenda kutuelekeza mazoezi na wachezaji wote tutayafanya kwa nguvu ili kwenda kufanya vizuri ugenini.

"Tunakwenda kurudiano nao kule Lubumbashi matokeo yoyote ambayo tutakutana nayo tupo tayari kuyakabili ili tunawahidi mashabiki wetu tutatambana mpaka jasho la mwisho ili kupata ambacho Mungu atakuwa ametupangia," alisema Coulibaly.

James Kotei alisema mechi hii ya nyumbani ilikuwa muhimu kwetu kupata matokeo ya ushindi kama ilivyokuwa katika mechi zote ambazo tumecheza nyumbani msimu huu katika mshindano haya ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Hatukuwa na bahati ya kufunga kwani tulipata nafasi za kufanya hivyo lakini ilishindikana, tunakwenda kufanya maandalizi ya mechi inayofata ya marudiano lengo ni kufanya vizuri na naimani tutakwenda kupata kile ambacho Mungu ametuandikia pale DR Congo," alisema Kotei.