Wasanii kuweni wakweli ili msaidiwe

Muktasari:

Mbali na jitihada hizo lakini pia, kuna matatizo ambayo huwa hayaepukiki iki-wamo kifo. Kwa hapa nchini wasanii kufariki dunia kwa mazingira ya kisiri inaelekea kuwa kawaida.
Baada ya mauti kumfika msanii, hakuna mtu anayebaki kuelezea mashabiki na jamii nzima kwa ujumla kilichotokea.

Maisha ya usiri yana uzuri na ubaya wake. Utaona ubaya wake utakapofikwa na shida lakini utaona uzuri wake utaka-pokuwa unafanya miradi inayowafaid-isha  wengi.
Kwa mfano, wasanii hapa nchini Tanzania wamekuwa na mchango mkubwa katika kuibadili nchi na kuonekana yenye vipaji mbalimbali kwenye ulingo huo.
Sanaa ya uigizaji wa filamu na nyimbo, imekua hadi anga za kimataifa, hakika hayo ni mafanikio kwa Taifa hili.
Nakumbuka katika enzi za uhai wa marehemu Steven Kanumba, Bongo Movie ilikuwa imeanza kutanua na kufi-ka kimataifa.
Upande wa muziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Fleva, wasanii wanajituma kweli kweli hata licha ya kujitokeza changamoto ndogo ndogo zi-nazoweza kuepukikwa.
Ukitaja muziki wa Bongo Fleva, ni sawa na Davido kutaja Naija Music na Jua Cali kuizungumzia Genge.
Mbali na jitihada hizo lakini pia, kuna matatizo ambayo huwa hayaepukiki iki-wamo kifo. Kwa hapa nchini wasanii kufariki dunia kwa mazingira ya kisiri inaelekea kuwa kawaida.
Baada ya mauti kumfika msanii, hakuna mtu anayebaki kuelezea mashabiki na jamii nzima kwa ujumla kilichotokea.
Kwa mfano, miaka kadhaa iliyopita, msanii Albert Mangwea maarufu kama Ngear, alifariki dunia akiwa Afrika Kusini kutokana na kile kilicholezwa kwamba alizidiwa
Baadaye, kuna wasanii ambao walifariki dunia akiwamo Side Boy, Mez B, Kanumba na wengine tu sana. Kati ya hao hakuna ambaye taarifa zake zilitoka zikiwa zimenyooka na za kuridhisha. Kila mtu anakuwa na historia yake ya jinsi alivyomfahamu marehemu na sababu zake kufariki.
Ikumbukwe kwamba Juni 7, 2018, msanii Sam wa Ukweli alifariki dunia, muda mfupi baada ya kuimba wimbo wake wa mwisho. Hapa hakuna ndugu, rafiki wala jamaa ambaye alikuwa ana ufahamu wa kuhusu kifo hicho, kila mtu alisema alivyofikiri. Je, unakumbuka jinsi Pancho Latino alivyoiga dunia akiwa ufukweni mwa bahari, yupo aliyefahamu kilichotokea? Hata waliokuwapo walitoa taarifa zilizotofautiana.
Hii ina maana gani? Ina maana kwamba wasanii wa Bongo wana kurasa nyingi za maisha yao. Mbali na kuonekana jukwaani wakidhihirisha uwezo na vipaji vyao, pia wana maisha ambayo labda ni ya chuki, uoga na ubinafsi.
Msanii wa muziki wa Rap nchini, Jacob Mbunda maarufu kama Godzilla, amefariki dunia wiki hii.
Msanii huyo ambaye alikuwa hodari kwenye miondoko ya kuchana alifariki dunia akiwa nyumbani kwao Salasala jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa dada wa marehemu, msanii huyo alifariki dunia baada ya ki-wango cha sukari kupanda.
Afadhali Godzilla maana mtu wake wa karibu alikuwa bega kwa bega wakati akichukuliwa vipimo na matibabu ingawa alifariki akiwa anaendelea na dawa.
Hata hivyo, bado kuna changamoto mi-ongoni mwa wasanii wetu. Kwa nini maradhi au masaibu yao wasiyaweke wazi wao kwa wao na hata ikiwezekana wawe na kikundi au vikundi maalumu vya kusaidiana?
Siku hizi, hadi kina mama wa vijijini wameunda vikundi vya kusaidiana wa-kati wa shida.  Hata hivyo, wasanii wetu hawa hususan wa muziki wamekuwa wabinafsi sana na maisha yao.
Huu ndiyo muda mwafaka wa wasanii nchini kuunda taasisi ndogo itakayokuwa maalumu kwa ajili ya kuwasaidia wakati wa matatizo kama vile maradhi, ajali na vitu vya dharura.
Nchi nyingine, wasanii wanaheshimika. Inapotolewa habari tu kwamba msanii kakuktwa na tatizo, kwanza makampuni mbali mbali yanamkimbilia kwa ajili ya kutoa msaada.
Hii inanirudisha nyuma kipindi cha maradhi ya msanii wa kuchekesha, Mzee Majuto. Nakumbuka kuna wakati aliom-ba msaada wa kimatibabu. Wengi ha-wakuamini kwamba msanii yule hakuwa na hela za kugharamia matibabu yake, lakini, kama wasanii hawa wangekuwa na taasisi au chama chao cha kusaidiana bila shaka mambo yao yasingekwama.
Baada ya msanii kutoka kulingana na kazi zake nzuri, anaamua kuanza kuiga maisha ya uzunguni na hapo ndiyo siri inapokuja. Huwezi kufanya siri kama huna uwezo wa kutosha kiuchumi.
Mmoja kati ya waandaji wa muziki mkoani Mwanza, H Pol, anasema wasa-nii wengi wamejenga mazoea ya kujisahau maishani na hivyo kuonekana tofauti kabisa panapotokea tatizo.

Uchambuzi huu umeandikwa na mwandishi wa gazeti la Mwananchi kutoka Mwanza anayepatikana kwa namba 0744205617