Wapiga kura Yanga washushwa presha

Muktasari:

  • Hata hivyo, baadhi ya wanachama wenye kadi za benki na wale wa zamani wenye kadi za vitabu walionyesha wasiwasi majina yao kuwepo katika leja.

BAADA ya Kamati ya Uchaguzi wa Yanga na ile ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutangaza watakaopiga kura Yanga watatambulika kutokana na leja ya klabu, baadhi ya wanachama waliingiwa hofu ya kukosa haki hiyo ya msingi.

Uamuzi wa kutumia leja umekuja baada ya baadhi ya wanachama kupinga mchakato wa uchaguzi huo kutambua kadi za benki kutumika.

Hata hivyo, baadhi ya wanachama wenye kadi za benki na wale wa zamani wenye kadi za vitabu walionyesha wasiwasi majina yao kuwepo katika leja.

“Huwezi kupewa kadi ya uanachama kabla ya kuingizwa katika leja, hivyo mwanachama kama alifuata utaratibu sahihi lazima atakuwa yuko kwenye leja,” alisema aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Lawrance Mwalusako.

Alisema utaratibu wa Yanga ulikuwa ni kuingizwa kwanza katika leja ndipo unapewa kadi ya uanachama, hivyo wanachama walifuata taratibu zote.