Wanyama hauziki Tottenham Hotspurs

Tuesday January 28 2020

Wanyama hauziki Tottenham Hotspurs- nahodha wa Harambee Stars -Victor Wanyama-Tottenham Hotspurs-Celtic klabu-

 

By Thomas Matiko

HATMA ya nahodha wa Harambee Stars Victor Wanyama katika klabu yake ya Tottenham Hotspurs inaendelea kuzua stori huku ripoti za sasa kutoka Uingereza zikidai kuwa klabu hiyo imeshindwa kumuuza.

Kulingana na Evening Standard Sports, Spurs imeshindwa kumpiga bei Wanyama kutokana na klabu hiyo kutaka kumuuza kwa bei ya ndege, jambo ambalo limeifanya klabu kadhaa kumchorea giza.

Msimu uliopita Spurs walikuwa wameweka thamani ya Wanyama kuwa pauni 17 milioni lakini klabu ya Ubelgiji Club Brugge ilipowajia na ofay a pauni 13.6 milioni, waliamua kushuka sababu hakuna klabu nyingine iliyokuwa imeonyesha nia ya kumnunua. Lakini licha ya kuafikiana bei, Wanyama hakuweza kujiunga na Brugge baada yake kushindwa kuafikiana suala la mshahara wake.

Club Brugge ilikuwa ikimtaka apunguze mshahara wake anaoupokea kwa sasa wa Pauni 65,000 (Sh8 milioni) kila wiki, jambo ambalo Wanyama hakupendelea na hivyo kuamua kuendelea kutumikia mktaba wake na Spurs hadi mwisho. Hatua hiyo inadaiwa ilimchukiza Mwenyekiti wa Surs Daniel Levy baada ya Wanyama kuganda kuuzwa.

Licha ya hilo, jitihada za kumuuza zimeendelea na ilitegemewa kwamba kwenye dirisha hili dogo la Januari.

Hata hivyo dalili zinaonyesha kwamba huenda hilo lisitokee zikiwa zimesalia siku nne tu dirisha lifungwe kwani mpaka sasa hamna klabu kati ya zilizovumishwa kumhitaji, imewasilisha ofa.

Advertisement

Celtic klabu aliyotokea akija Uingereza pia ilikuwa imeonyesha dalili lakini baada ya kumtaka Wanyama apunguze mshahara wake, akaganda tena.

Sasa ili kurahisha mahesabu kutokana na hali hiyo Spurs wamelazimika kupunguza dau la Wanyama na sasa wanaomba Pauni 9 milioni pekee kwa klabu itakayom hitaji.

Spurs walitegemea wagentengeza faida zaidi kwa zile senti walizotumia kumsajili Pauni 11 milioni 2016 kutoka Southampton ila matakwa yake ya kimshahara ndio imeifanya biashara kuwa ngori.

Mkataba wa Wanyama umesalia na miezi 18 pekee.

Advertisement