Wanyama awabeba nyota 23 wa Kenya fainali za Afcon

Muktasari:

Kenya imepangwa Kundi C pamoja na Algeria, Senegal na Tanzania. Harambee Stars itaanza fainali hizo Juni 23 kwa kuivaa Algeria kwenye Uwanja wa 30 June, Cairo.

Cairo, Misri. Kocha wa Kenya Mfaransa, Sebastien Migné ametangaza kikosi chake cha wachezaji 23, chini ya nahodha Victor Wanyama tayari kwa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON), Misri.

Kenya imepangwa Kundi C pamoja na Algeria, Senegal na Tanzania. Harambee Stars itaanza fainali hizo Juni 23 kwa kuivaa Algeria kwenye Uwanja wa 30 June, Cairo.

Kiungo wa Zesco United, Teddy Akumu ameachwa katika kikosi hicho pamoja na nyota wa Olimpico Montijo,s Clifton Miheso. Chris Mbamba na beki Brian Mandela wameachwa kwa sababu ya kuwa majeruhi.

Kikosi:

Makipa: Patrick Matasi (St. George, Ethiopia), Faruk Shikalo (Bandari FC), John Oyemba.

Mabeki: David Owino (Zesco United, Zambia), Musa Mohammed (Nkana FC, Zambia), Bernard Ochieng (Vihiga United) Joseph Okumu (Real Monarch, USA), Joash Onyango, Philemon Otieno (Gor Mahia, Kenya), Eric Ouma (Vassalund, Sweden), Aboud Omar (Sepsi OSK, Romania).

Viungo: Victor Wanyama (Tottenham Hotspur, England), Ismail Gonzalez (UCD Las Palmas, Spain), Dennis Omino (Sofapaka FC), Eric Johannah (IF Bromma, Sweden), Francis Kahata (Gor Mahia, Kenya), Paul Were (AFC Leopards), Johannah Omolo (Cercle Brugge, Belgium).

Washambuliaji: Ovela Ochieng (Vassalund, Sweden), Ayub Timbe (Beijing Renhe, China), Michael Olunga (Kashiwa reysol, Japan), John Avire (Sofapaka, Kenya), Masud Juma (Al Nasr, Libya).