Wametupia nne, tano England

LONDON, ENGLAND. Mkorea Heung-min Son amewavuruga Southampton juzi Jumapili wakati alipofunga mara nne peke yake kuisaidia Tottenham Hotspur kushinda 5-2 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England.

Utamu wa mechi hiyo ni kwamba Spurs ilishinda ugenini, huku mabao yote manne ya Son aliyeasisti ni Harry Kane, ambaye pia alisukumia wavuni bao jingine la miamba hiyo inayonolewa na Mreno Jose Mourinho. Kane na Son walitengeneza kombinesheni iliyoonekana kuwa ni shida kubwa kwa mabeki wa Southampton.

Hata hivyo, staa huyo wa kimataifa wa Korea Kusini sio mchezaji wa kwanza kufunga mabao yanayoanzia manne na kuendelea kwenye mchezo mmoja wa Ligi Kuu England baada ya kuwapo wengine kibao.

1.Efan Ekoku

(Everton)

1-5 dhidi ya Norwich, Septemba 1993.

2.Andy Cole

(Man United) – 9-0 dhidi ya Ipswich, Machi 1995 (amefunga matano), 5-1 dhidi ya Newcastle, Agosti 1999.

3.Robbie Fowler (Liverpool) – 5-2 dhidi ya Bolton, Septemba 1995 na 5-1 dhidi ya Middlesbrough, Desemba 1996.

4.Gianlucca Vialli (Chelsea) – 0-6 dhidi ya Barnsley, Agosti 1997.

5.Jurgen Klinsmann (Tottenham) – 2-6 dhidi ya Wimbledon, Mei 1998.

6.Michael Owen (Liverpool) – 5-1 dhidi ya Nottingham Forest, Oktoba 1998 na 0-6 dhidi ya West Brom, Aprili 2003.

7.Ole Gunnar Solskjaer (Man United) – 1-8 dhidi ya Nottingham Forest, Februari 1999 na 5-1 dhidi ya Everton, Desemba 1999.

8.Alan Shearer (Newcastle) – 8-0 dhidi ya Sheffield Wednesday, Septemba 1999 (amefunga matano).

9.Jimmy Floyd Hasselbaink (Chelsea) – 6-1 dhidi ya Coventry, Oktoba 2000.

10.Mark Viduka (Leeds) – 4-3 dhidi ya Liverpool, Novemba 2000.

11.Thierry Henry (Arsenal) – 5-0 dhidi ya Leeds, Aprili 2004.

12.Yakubu Portsmouth na Blackburn) – 5-1 dhidi ya Middlesbrough, Mei 2004 na 4-2 dhidi ya Swansea, Desemba 2011.

13.Dimitar

Berbatov (Spurs na Man U) – 6-4 dhidi ya Reading, Desemba 2007 na 7-1 dhidi ya Blackburn, Novemba 2010 (amefunga matano).

14.Frank Lampard (Chelsea) – 6-1 dhidi ya Derby, Machi 2008 na 7-1 dhidi ya Aston Villa, Machi 2010

15.Andrey

Arshavin

(Arsenal) – Andrey Arshavin dhidi ya Liverpool

16.Robbie Keane (Tottenham) – 5-0 dhidi ya Burnley, Septemba 2009

17.Jermain Defoe (Tottenham) – 9-1 dhidi ya Wigan, Novemba 2009 (amefunga matano)

18.Wayne Rooney (Man United) – 4-0 dhidi ya Hull, Januari 2010

19.Louis Saha (Everton) – 5-3 dhidi ya Blackpool, Februari 2011

20.Edin Dzeko (Man City) – 1-5 dhidi ya Tottenham, Agosti 2011

21.Luis Suarez (Liverpool) – 5-1 dhidi ya Norwich, Desemba 2013

22.Sergio Aguero (Man City) – 4-1 shisi ya Tottenham, Oktoba 2014, 6-1 dhidi ya Newcastle, Oktoba 2015 (amefunga matano) na 5-1 dhidi ya Leicester City, Februari 2018.

23.Geor ginio Wijnaldum (Newcastle) – 6-2 dhidi ya Norwich, Oktoba 2015

24.Romelu Lukaku (Everton) – 6-3 dhidi ya Bournemouth, Februari 2017

25.Harry Kane (SPURS) – 1-6 dhidi ya Leicester, Mei 2017

26.Mohamed Salah (Liverpool) – 5-0 dhidi ya Watford, Machi 2018

27.Michail Antonio (West Ham) – 0-4 dhidi ya Norwich, Julai 2020

28.Heung-min Son (Tottenham) – 2-5 dhidi ya Southampton, Septemba 2020.