Wamedamshi kinoma yaani!

Muktasari:

Katika ulimwengu wa muziki wa sasa, wasichana maarufu kwa jina la Video Queens wana umuhimu mkubwa lakini sasa Kibongobongo inashangaza kuona baadhi  ya wanamuziki wanashindwa kutoa nyimbo nzuri ili kuwatumia vizuri katika video zao.

Wasanii wengi wa Muziki wa Bongo Fleva, kila wanapotoa nyimbo mpya hufikiria pia kuutengenezea video kali ili kuweza kuwashika vilivyo mashabiki zao. Katika video hizo, wapo wanaofikia hatua ya kwenda kuzifanyia nje ya nchi, Lakini sasa, kwenye uandaaji wa video hizo kuna watu muhimu sana ambao wamekuwa wakitumika kuzifanya ziwe na mvuto wa kutazamwa.
Watu hao ni wasichana wakali wanaofahamika kwa jina la Video Queens. Katika ulimwengu wa muziki wa sasa, wasichana hawa wana umuhimu mkubwa lakini sasa Kibongobongo inashangaza kuona baadhi  ya wanamuziki wanashindwa kutoa nyimbo nzuri ili kuwatumia vema katika video zao.
Wapo pia mavideo Queens ambao wakichaguliwa kunogesha video za wanamuziki wanashindwa kutendea haki video hizo, ila kwa hapa Mwanaspoti linakuletea mavideo Queens ambao waliowahi kunogesha video za wanamuzki na kusababisha hiyo video ikiwemo na wimbo wake kupendwa na mashabiki huku ukifanya vizuri sokoni.

Vera Sidika
Huyu ni video Queen mwenye umbo matata,yuko vizuri kwenye kunogesha video za wanamuziki,na aliweza kufanya vizuri katika wimbo wa Hamornize ‘Show Me’ na kusababisha kutusua kinoma.
Ni  mrembo kutoka Kenya,ambaye mwenye vipaji kama Utangazaji,mwanamitindo na video Queen .Anapenda maisha ya juu na ya raha; na hiyo ni gharama ambayo wanaume wengi wa Kenya,Tanzania mara nyingi hushindwa  kuzimudu na wababakia mate kuwadondoka tu.
Video ya wimbo wa ‘Show Me’ ilipata kuvuma sana kutokana na mwanadada Vera Sidika amejipatia umaarufu Tanzania kuitendea haki kwa kulichezesha vema umbo lake huku akitoa mauno ya haja.
Mpaka sasa ngoma hiyo imetazamwa na watu 10,549,125 tangu ilipowekwa kwenye mtandao Aprili 16,2017.

Masogange
Huyu pia alikuwa mmoja wa Mavideo Queen matata katika kunogesha video za wanamuziki kwa sasa ni marehemu, Agnes Gerald a.k.a Masogange alipata umaarufu baada ya kuuza sura kwenye video ya Belle 9 na wimbo wa ‘Masogange’na hadi anafariki jina lake maarufu ni Masogange ikiwa jina lake halisi ni Agnes Gerald.
Masogange aliweza kuipush video ya wimbo wa masogange kutokana na kuwa na umbo lenye mvuto na lenye kuendana na mashairi ya wimbo huo.Na Belle 9 aliuweka katika Youtube Oktoba 25, 2011 na hadi sasa umetazamwa na watu 550,636.

Zari
Ni mfanyabiashara maarufu na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz,jina maarufu ni  Zari The Bosslady.Zari amewahi kushiriki kwenye video ya ngoma ya Diamond ‘Utanipenda’ miaka mitatu iliyopita.
Video ya utanipenda ilifanya vizuri na kwenye mtandao wa Youtube mpaka jana imetazamwa na watu 13,617,017 tangu ulipowekwa kwenye mitandao Desemba 11,2015. Wimbo huo ulikuwa na maana kubwa kwenye penzi la Zari na Diamond, ambapo ulianza kunogeshwa kwa kiki kuwa wawili hao wamefunga ndoa kutokana na mazingira na mavazi yaliyotumika kurekodia.
‘Je Utanipenda’ ni wimbo ambao unazungumzia Diamond pindi atakapofilisika maisha yake kuwa hayaelewiki je Zari atampenda? Hapo ndipo Zari aliweza kutenda haki kutokana na mshairi ya wimbo huo na kuufanyta kutamba kinoma.

Jike Shupa
Huyu ni mwanadada wa kimjini sana,hapo mwanzo aliwahi kuwika baada ya kutoka kimapenzi na Juma Nature na kujaaliwa kupata mtoto, lakini Nuh Mziwanda, ambaye alikuwa ametoka kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu, Shilole alimuibua na kumfanya Video Queen wake kwenye ngoma ya Jike Shupa.
Video ya Jike Shupa iliwabamba mashabiki kinoma kwani, ilikuwa ikiangazia zaidi matukio na namna Nuh alivyokuwa akiteseka kwenye hilo penzi lake, ambapo Jike Shupa alitenda haki hasa ikizingatiwa kuwa umbo lake lilitosha kumdhibiti Nuh kwa vipigo kila kukicha.
Wakati ngoma hiyo ikianza kupoteza mvuto, Jike Shupa ameendelea kutumia jina hilo na kumfanya kuwa maarufu zaidi kwenye mitandao ya kijamii. Ngoma ya Jike Shupa iliwekwa rasmi mtandaoni Juni 10, 2016 na mpaka kufikia jana jioni ilikuwa imetazamwa na watu 2,924,571.
Wakati ngoma hiyo ikitamba, kukaibuka zogo baada ya watu kudai kuwa wimbo huo unaashia kuwa ni dongo kwa Shilole, ambapo mwanadada huyo hakukubali na kuamua kuingia studio kupika ngoma ya Dume Dada kujibu mapigo ya Jike Shupa.

Nargis
Kama unakumbukumbu mwaka 2012,mwanamuziki na ambaye pia Mbunge wa Mikumi Profesa Jay, alitamba kinoma na ngoma ya Zali la Mentali akimshirikisha Juma Nuter huku mshiriki wa Miss Tanzania 2004, Nargis Mohamed akipamba video ya wimbo huo pamoja na kupiga mistari pia.
Nargis, ambaye alikuwa mshindi wa tatu katika la Miss Tanzania alinogesha ngoma hiyo na kumfanya kuzidi kuwa maarufu.
Profesa Jay aliiweka Zali la Mentali Oktoba 10,2013 na mpaka sasa imeangaliwa na watu 1,688,568 kwenye mtandao wa Youtube.

Hamisa Mobetto
Wimbo wa Salome unatajwa kuwa ulikuwa mwanzo wa penzi la Diamond na Hamisa Mobetto, ambapo mwisho wa siku walipeana zawadi ya mtoto wa kiume, Dylan ambaye amekuwa maarufu kinoma kwa sasa kuanzia kwenye mitandao ya kijamii n ahata mitaani.
Kwanini? Dylan ndio alisababisha wazazi wake hao kupelekana mahakamani ambapo, Diamond alikilazimishwa kuwajibika kwa malezi ya mtoto huyo na staa huyo wa Bongo Flava alitinga viwanja vya Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam. Akiwa mahakamani hapo, Diamond ghafla tu akatengeneza headiline kwa kukatikiwa viatu na kumfanya kutembea peku mguu moja.
Lakini, Salome ilimbana kinoma na huko kwenye Youtube imeangaliwa na watu 26,856,973 hadi kufikia jana jioni.
Mpaka sasa baadhi ya mashabiki wamekuwa wakimuita Hamisa kwa jina la Salome kutokana na ngoma hiyo ambayo iliwahi kuimbwa na msanii wa ngoma za asili, Saida Karoli kufanyiwa remix na kuongezwa vionyo vya kisasa ambapo, Dimoand alimsgirikisha Rayvann.