Wamasai wateka uzinduzi uwanja wa Gwambina

Muktasari:

Uwanja wa Gwambina unazinduliwa leo kwa mechi ya kirafiki itakayopigwa saa 10:00 jioni katika dimba hilo.

WANANCHI  jamii ya Masai leo Ijumaa wameiteka Wilaya ya Misungwi katika sherehe za uzinduzi wa Uwanja wa Gwambina zinazoendelea kushika kasi wilayani hapa.
Masai hao ambao wametinga viwanjani hapo wakiwa wamevaa wa mavazi yao ya asili, wamegeuka kivutio na kupewa nafasi ya kuimba nyimbo za dini.
Uwanja wa Gwambina unazinduliwa leo kwa mechi ya kirafiki itakayopigwa saa 10:00 jioni katika dimba hilo.
Tayari Simba waliwasili tangu asubuhi ya jana Alhamisi ikiwa na baadhi ya nyota wake wakiwemo kipa Deogratius Munishi 'Dida',  Said Ndemla, Rashid Juma, Hassan Dilunga pamoja na wengine wa kikosi B ambao watakipiga na Gwambiana FC.
Gwambina inajiandaa kushiriki Ligi Daraja la Kwanza huku Simba wakijiandaa na Ligi Kuu pamoja na michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.