Wakenya, Mtanzania kuchezesha AFCON, Ghana

Muktasari:

Gor Mahia ilipata fursa ya kuwa timu ya kwanza kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kwenda nchini Uingereza kucheza mechi ya kuwania kombe dhidi ya klabu yenye hadhi kubwa kama Everton, baada  ya kutetea ubingwa wao wa kombe la Sportpesa kwa kuifunga SImba SC ya Tanzania 2-0, ugani Afraha, Nakuru, mapema mwaka huu.

Nairobi, Kenya. Waamuzi wawili kutoka Kenya, Caroline Wanjala na Mary Njoroge na Mtanzania, Jonesia Kabakama, ni miongoni mwa waamuzi 32, walioteuliwa na shirikisho la soka nchini humo, kuchezesha michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake, itakayotimua vumbi kuanzia Novemba 17 hadi Desemba mosi, mwaka huu, nchini Ghana.

Mwamuzi huyo Mtanzania hivi karibuni ndiye aliyechezesha mechi ya Simba na Yanga iliyoisha kwa suluhu bila ya kufungana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kabakana na Wanjala wametueliwa katika orodha ya waamuzi wa kati 16, huku Njoroge yeye akipenya katika orodha hiyo ya mapilato 32, kama mmoja wa waamuzi wasaidizi, ambapo kwa mujibu wa taarifa rasmi ya CAF, waamuzi hao 32, watafanya kozi ya siku nne, kabla ya michuano hiyo kutimua vumbi.
Kozi hiyo  ni ya kivitendo na nadharia, yataanza kuanzia Oktoba 17 hadi 21, katika mji wa Cape Coast, nchini Ghana. Taarifa hiyo ilieleza kuwa, moja ya maeneo yatakayozingatiwa katika kuwanoa waamuzi hao ni pamoja na tathmini ya mbinu za kiufundi, kupitia mkanda wa video ya mechi zilizopita, pamoja na maswala ya uadilifu.
“Kozi hii ni muhimu kwani inalenga kuwaandaa waamuzi na majukumu yao. Hii itasaidia sana kupunguza matukio ya uvunjifu wa sheria, pia tunalenga kuhakikisha wanaelewa umuhimu wa kuwa wadilifu,” alisema Meneja wa waamuzi wa CAF, Eddie Maillet.