Wakazi watano washinda Sh161.5 milioni za M-Bet

Muktasari:

Washindi hao ni Meshack Ngole (24) mkazi wa Mafinga, mkoani  Iringa, Musa Zubeli (24) mkazi wa Dar es Salaam, Lucas Zunzu (34), Kibamba (DSM), Saidi Ali (Zanzibar) na Juma Mganga wa Tanga.

Dar es Salaam. Jumla ya washindi watano wameshinda jumla ya Sh161, 467,950 baada ya kubashiri kwa usahihi droo ya kampuni ya M-Bet ijulikanayo kwa Perfect 12 inayoendelea nchini.

Washindi hao ni Meshack Ngole (24) mkazi wa Mafinga, mkoani  Iringa, Musa Zubeli (24) mkazi wa Dar es Salaam, Lucas Zunzu (34), Kibamba (DSM), Saidi Ali (Zanzibar) na Juma Mganga wa Tanga.

Akizungumza mara baada ya kuwakabidhi washindi hao jana, Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa washindi hao wameongeza idadi ya watanzania ambao mpaka sasa wamefaidika na michezo ya kubahatisha ya kampuni hiyo.

Mushi alisema kuwa wamefarijika sana kuona Watanzania wengi wanajitokeza zaidi kubashiri katika michezo yao na kuwainua kipato na maisha vile vile.

“Nilisema kuwa M-Bet ni nyumba ya mabingwa, hii imedhihirika ambapo washindi wanazidi kupatikana kupitia mchezo wetu wa Perfect 12, leo (jana) tumepata washindi watano ambao wamegawana dau la Sh milioni 161.4 na kila mmoja amejipatia Sh milioni 32, ni faraja kubwa kwani kwa Sh1,000 tu, unatengeneza faidi kubwa,”

“Nawaomba Watanzania ambao hawajaanza kubeti na M-Bet, waanze sasa kwani ni nyumba ya mabingwa ina wasubiria,” alisema Mushi.

Mmoja wa washindi hao, Meshack Ngole alisema kuwa hakuamini kama ameshinda kiasi hicho cha fedha na kudhani simu aliyopigiwa ilikuwa ya wale ‘wajanja’ wa mjini.

“Nilipoitwa ofisini na kuambiwa mambo ya kungua akaunti na masuala mengine, nilipumua na kufuta usemi kuwa washindi wengi wa fedha wa michezo ya kubashiri wanatengenezwa,” alisema Ngole.

Alisema kuwa atazitumia fedha hizo kwa ajili ya kujenga nyumba, kuhimarisha biashara zake na kusaidia ndugu zake.