Wagosi wala hawana presha

Friday April 3 2020

Wagosi wala hawana presha,MABOSI wa Coastal Union 'Wagosi wa Kaya,Ligi Kuu ,Daraja la Kwanza,

 

By Denis Chambi,Tanga

MABOSI wa Coastal Union 'Wagosi wa Kaya' wanajivunia kikosi kipana walichonacho na hata kama ikitokea mchezaji wao akitimkia timu nyingine hawana presha.
Hayo yanakuja baada ya kuwepo kwa taarifa za uhakika kwamba beki wao tegemezi, Bakari Mwanyeto anasaini Simba na wameshakubaliana ishu karibu zote.
Meneja wa timu hiyo, Iddi Kuha alisema; "Mpaka sasa hatuna wasiwasi  na wacheazaji wetu kwa nafasi tuliyopo inaonyesha wanapambana tunao wachezaji wengi hivyo hata kama wakiondoka baadhi yao bado tunao uwezo wa kufanya makubwa zaidi wala hatutoyumba.”

Advertisement