Wadau wafunguka Kariakoo Derby

Wednesday September 30 2020
wadau derby pic

Mechi ya watani wa jadi Yanga dhidi ya Simba imebakiza sikuu kadhaa ipigwe huku Yanga akiwa nyumbani, wadau wa soka wamechambua vikosi hivyo kuelekea mechi hiyo ambayo ni miongoni mwa dabi kubwa Afrika.

Beki wa zamani wa Simba na Taifa Stars, Boniface Pawasa amesema licha ya Yanga kupata ushindi kwenye mechi hizo bado timu yao haijakaa sawa na hata ushindi huo unampa shaka.

Ingawa anakiri kwamba, mechi ya watani hainaga ufundi mwingi wala mwenyewe kwa kuwa, habati nayo uhusika kuamua matokeo.

“Nimecheza kwa miaka mingi kama beki wa kati, nikimuangalia Mwamnyeto na Lamine staili yao ni moja ya uchezaji, Yanga wamekosa kiongozi ambaye ni mtulivu. Wana watu wazuri wa kuhangaika ila wakikutana na mastraika watulivu inaleta shida.

“Tatizo la washambuliaji wao kutofunga kama ilivyo kwa Simba nadhani ni mbinu za mwalimu, amewakuta wachezaji tayari wamesajili hivyo sio rahisi kwa haraka kuwafanya wacheze kama amavyotaka, bado wapewe muda,” alisema Pawasa ambaye kwa sasa ni kocha wa soka la ufukweni.

Naye Herry Morris alisema Zlatko anatakiwa kuwapigisha msasa nyota wake ili kuongeza kasi ya umaziliaji wa mabao ambao unaonekana kuwa tatizo kubwa kwa mpaka sasa.

Advertisement

“Yanga wanaweza kutengeneza nafasi tano za mabao lakini, zikapotea zote bila kuzamisha nyavuni. Kufunga kwa Lamine ni jambo zuri ila wawepo wengine wa kufunga ili kuongeza wigo zaidi, wana timu nzuri ila haijakaa sawa,” alisema.

Kocha wa Biashara alikiri Simba ina fowadi matata zaidi VPL msimu huu, huku Mkurugenzi wa ufundi wa Gwambina, Mwinyi Zahera akidai Simba inaonekana kuwa imara zaidi kwa vile inakutana na timu ambazo hazijaimarika msimu huu.

Advertisement