Wadau wa soka wajitokeza kumzika Said Mrisho

Muktasari:

  • Mrisho alifariki akiwa njiani kwenda kwnye matibabu ambayo yalikuwa yakigharamiwa na wachezaji veterani waliochangishana kupitia umoja wao.

Dar es Salaam.Wadau mbalimbali wa soka nchini wamejitokeza kwenye mazishi ya nyota wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Said Mrisho yaliyofanyika Leo Jumatano.
Mazishi ya Mrisho yamefanyika baada ya swala ya Alasiri nyumbani kwao Kilosa nje kidogo ya mji wa Morogoro.
Mrisho alifariki Jana Jumanne akiwa Mikese safarini kupelekwa Dar es Salaam kwenye matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua vidonda vya tumbo.
Mrisho aliyekuwa mshambuliaji mwenye kiwango bora Yanga na Stars amezikwa Leo katika mazishi yaliyoudhuliwa na wadau mbalimbali wa soka.
Miongoni mwa wadau hao ni John Simkono, Salum Mayanga, Mohamed Ndunda, Ally Jangalu na Hussein Ngulungu.
Pia Mwenyekiti wa Chama cha Wachezaji Veterani nchini (OMSOTA), Paul Lusozi alikuwa miongoni mwa walioshiriki katika mazishi hayo.
Akimzungumzia Mrisho, Ngulungu ambaye alikuwa miongoni mwa nyota walioshiriki AFCON alisema Mrisho alikuwa na mchango mkubwa katika soka nchini enzi akicheza.