Wadau Olimpiki kushiriki kongamano la michezo Dar

Friday June 26 2020

By Imani Makongoro

Dar es Salaa. Viongozi wa vyama na mashirikisho ya michezo nchini yaliyo kwenye mfumo wa Olimpiki ni miongoni mwa wadau watakaoshiriki Kongamano la michezo litakalofanyika kesho Jumamosi.
Kongamano hilo linalenga kujadili athari na changamoto zilizoikabiri sekta ya michezo nchini wakati huu wa janga la corona.
Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Henry Tandau alisema kongamano litafanyika kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Amesema litashirikisha viongozi wa michezo wa mashirikisho, ambayo yako katika mfumo wa Olimpiki pamoja na waandishi wa habari za michezo nchini wasiopungua 60.
"Tutakuwa na mjadara mpana juu ya athari ambazo zimeikuta tasnia ya michezo wakati huu wa corona, tulitarajia kuwa na washiriki wengi zaidi, lakini tumeweka idadi hiyo ili kuchukua tahadhari ya janga la corona.
Olimpiki ni miongoni mwa matukio ambayo yameathiriwa na corona mwaka huu baada ya michezo hiyo iliyokuwa ianze Julai kuahirishwa hadi mwakani.

Advertisement