Wachina wampa Gareth Bale ofa ya kufuru

Tuesday July 23 2019

 

KLABU ya Beijing Guoan ya China imeweka mezani dau la Pauni 1 milioni kwa wiki kwa staa wa kimataifa wa Wales, Gareth Bale na endapo staa huyo atakubali dau hilo atakuwa mchezaji anayelipwa zaidi duniani kwa sasa.

Bale ameonyeshwa mlango wa kutokea na Real Madrid baada ya juzi Kocha Zinedine Zidane kudai staa huyo anakaribia kuondoka Santiago Bernabeu na ndio maana hakumpanga katika mechi ya kirafiki dhidi ya Bayern Munich.

Licha ya kuwa na ofa kutoka China inadaiwa staa huyo anatakiwa kwa nguvu zote na klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani ambayo imepoteza mawinga wake wawili, Franck Ribery na Arjen Robben walioachana na klabu hiyo.

Bale Kocha Zidane wanaonekana kutokuwa na uhusiano mzuri ingawaje wawili hao wamekuwa wakikanusha mara kwa mara kwamba hakuna tatizo kati yao.

Advertisement