Wachezaji tenisi Taifa matatani

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwananchi jana, Ofisa wa Habari wa BMT Najaha Bakari alisema viongozi wa Chama Tenisi Tanzania (TTA) ulitakiwa kuomba kibali kabla ya siku 14.

Dar es Salaam.Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limesema timu ya Taifa ya baiskeli ya tenisi ilikwenda Kenya kinyume cha sheria.

Timu ya Taifa ipo Kenya kushiriki mashindano ya kutafuta nafasi ya kufuzu kucheza mashindano ya dunia nchini Israel Mei Mosi, mwaka huu

Wachezaji waliokwenda kushiriki mashindano hayo ni Rehema Selemani , Lucy Julias, Juma Hamisi na Novatus Temba ambao wako chini ya kocha Salumu Mvita.

Akizungumza na Mwananchi jana, Ofisa wa Habari wa BMT Najaha Bakari alisema viongozi wa Chama Tenisi Tanzania (TTA) ulitakiwa kuomba kibali kabla ya siku 14.

“Kimsingi kama walikuwa na barua ya mwaliko wa mashindano wangeleta kopi wakiambatanisha na barua ya kuomba kibali,” alisema Najaha.

Ofisa Habari huyo alisema wanatarajia kuwaita viongozi wa TTA kutoa maelezo ya kupeleka timu nje ya nchi bila kibali.