Wachezaji Simba wamlilia Mo Dewji

Thursday October 11 2018

 

By Oliver Albert

Dar es Salaam. Wachezaji na wasanii mbalimbali wameonekana kuguswa na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu na mfadhili wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji 'Mo'.
Mo alitekwa leo Alhamis asubuhi wakati akielekea kwenye hotel ya Colosseum, kwa ajili ya kufanya mazoezi gym.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa  alisema Mo  alitekwa na wazungu wawili .
"Leo asubuhi wazungu wawili walikuwa na gari aina ya suff. Kulikuwa na magari mawili, gari moja lilikuwa ndani na lingine lilikuwa nje, gari la ndani liliwasha taa ghafla na lile lililokuwa nje likaingia na kwenda kupaki karibu na gari la MO Dewji lililokuwa limepaki na wakati akishuka wazungu wawili  wakatoka na kumbana MO  Dewji baada ya kutoka ndani ya gari lake, na kisha kumpakia katika gari lao aina ya suff na kuondoka naye." alisema Mambosasa.
Wachezaji Simba na wasanii wameposti katika mitandao ya kijamii wakimtakia usalama tajiri huyo kijana Afrika.
Aishi Manula-Ewe mola wetu (allah) mfanyie wepesi Mo Dewji kwenye mapito na mtihani alioupata,mfanye awe mwenye kuyashinda mapito hayo na kuwa huru.
Kichuya- Mungu akulinde uwe salama,Amen  Mo Dewji
John Bocco -Mungu akusimamie na kukulinda huko ulipo inshaallah.. atakuepusha na changamoto zote na kurudi salama
Shomary Kapombe - Ee Mungu nenda ukamtie nguvu na kumlinda na awe katika ushindi kwenye hili Mo Dewji tunakuombea na Mungu atakufanyia wepesi.
officiall_mussamgosi:Vilio vya wana simba yarabi tunakuomba habari yoyote ikija isiwe mbaya na na nyoyo zetu yarabi unazishuhudia zinavyo pata maivu mpe ujasiri na nguvu ya kumponya ktk hili inshaallah mungu atamfanyia wepesi.
Officialmeddiekagere:Mwenyezi Mungu akuepushe na hatari zote urejee salama Boss @moodewji 🙏🙏
Emmanuel Okwi -Kila kitu kitakuwa sawa Mo Dewji
Jacquline Wolper- Mwenyezi Mungu akawe ngao yako baba,binadam si kitu chini ya jua,jemedali ni mmoja tuu hakuna mwenye vitisho wala mamlaka kumzidi yeye.Tupo nyuma yako.
Steve Nyerere-Pole familia,najua na kutambua kila  mtu sasa hivi anaongea lake,cha muhimu ni kuwapa ushirikiano Jeshi letu la polisi ,kaka yetu ,rafiki yetu apatikane .Jambo kama hili halina ushabiki wa Simba wala Yanga wote tunaungana kumuombea Mo Dewji apatikane akiwa salama. Mungu ibariki Tanzania. Amina.

Advertisement