Wabrazil waliamsha Simba

Muktasari:

Katika mchezo huo na Bandari, Wilker alicheza mshambuliaji wa mwisho akisaidiwa Ibrahim Ajibu na Mkenya Frances kahata. Mbali na Wilker, lakini Wabrazili wengine wawili Tairone Santos na Gerson Fraga walianza kwenye mchezo huo.

KWA wa mara ya kwanza mashabiki wa Simba wanamshuhudia nyota wao watatu wa Kibrazili wakianza pamoja baada ya Wilker Da Silva kuanza  kwenye mchezo wao wa kirafiki na Bandari FC ya Kenya ambao ulimaliza dakika 45 kwa suluhu.
Walker ambaye alikuwa nje kwa kipindi kirefu kutokana na maumivu ya goti tangu alipoumia kwenye mechi ya kujipima nguvu na Orlando Pirates nchini Afrika Kusini.
Tangu hapo alikuwa nje na hata alipopona hakupata nafasi ya kucheza mechi ya Ligi Kocha Kocha Patrick Aussems aliweka wazi ni kama hakuwa tayari kwa sababu alitaka kumchezesha mechi na Biashara United akaumia tena akiwa mazoezini.
Katika mchezo huo na Bandari, Wilker alicheza mshambuliaji wa mwisho akisaidiwa Ibrahim Ajibu na Mkenya Frances kahata. Mbali na Wilker, lakini Wabrazili wengine wawili Tairone Santos na Gerson Fraga walianza kwenye mchezo huo.
Alicheka kwa kutumia nguvu na kulazimisha mashambulizi kwa wapinzani wao Bandari hata hivyo safu yao ya ulinzi ilikuwa imara.
Hata hivyo, Aussems alimjaribu dogo wa U-20, Joseph Peter kucheza beki wa kushoto huenda ni kwa sababu Mohammed Hussein 'Tshabalala' na Gadiel Michael ambao wako na Taifa Stars nchini Rwanda wanakocheza mechi ya kirafiki na Amavubi.
Hata hivyo,  Peter alicheza dakika 45, nafasi yake ikachukuliwa na Yusuf Mlipili.

MCHEZO ULIVYOKUWA
Dakika ya 42, Berno Kakolanya amecheza vizuri shuti ya William Wadri  ukatoka nje nakuwa kona.
Dakika ya 43, Simba walifanya shambulio zuri kupitia kwa Frances Kahata akampasia Ajibu lakini shuti lake lilimlenga kipa wa Bandari akadaka.
'MOLINGA' AIBUKA
Kama ilivyo utani wa jadi mshabiki wa Simba wamempachika jina straika wa Bandari, Wycliffe Ochomo jina la mshambuliaji wa Yanga,  David Molinga.
Straika humor kimwonekano ana mwili mkubwa kama ambavyo Molinga alivyo na huenda ndio sababu wakampa jina hilo na hata anavyocheza anatumia nguvu.
Kwa sasa mchezo upo zaidi ya dakika 60 na matokeo bado ni 0-0.