Wabongo wapata neema Afcon

Muktasari:

Waziri Mkuu Majaliwa ambaye  ni mgeni rasmi katika Sherehe hizi za ufunguzi wa Fainali za Afcon na alipopewa nafasi ya kuzungumza ndio alisema, kuanzia kesho watanzania wote watapata uhuru wa kuingia uwanjani bure kwenda kuangalia fainali hizo.

 WATANZANIA wamejikuta wameangukiwa na neema katika Fainali za Vijana (AFCON) chini ya miaka miaka 17, baada ya Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri wa Muungano Tanzania, Kassim Majaliwa kutangaza Watanzania wote kuingia uwanjani bure kuangalia Mashindano hayo kuanzia kesho Jumatatu.

Waziri Mkuu Majaliwa ambaye  ni mgeni rasmi katika Sherehe hizi za ufunguzi wa Fainali za Afcon na alipopewa nafasi ya kuzungumza ndio alisema, kuanzia kesho Watanzania wote watapata uhuru wa kuingia uwanjani bure kwenda kuangalia fainali hizo.

"Sisi kama Serikali tunasema kuanzia kesho watanzania wote wataingia bure Uwanjani, Tanzania Oyee," alimalizia kwa kusema hivo.

Idadi ya ndogo ya mashabiki waliojitokeza uwanjan ileo, inatajwa sababu ya Waziri Mkuu kutangaza kutokuwa na kiingilio ili kuongeza nguvu ya mashabiki uwanjani.