Wababe wa Yanga kuwanoa Simba

Muktasari:

  • Simba inajiandaa na michuano ya Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza Agosti 23 mwaka huu pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika ikiiwakilisha Tanzania baada ya kutwaa ubingwa wa ligi msimu uliopita.

WAKATI klabu ya Simba ikiwa inaendelea na kambi yake ya maandalizi kwaajili ya msimu ujao nchini Afrika Kusini, benchi la ufundi limepanga kucheza mechi tatu za kirafiki.
Mechi ambayo tayari imethibitoshwa ni ile itakayochezwa Julai 17 mwaka huu dhidi ya Township Rollers ya Botswana huku wakiendelea na mazungumzo timu zingine kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki zitakazochezwa Julai 23 na 30.
Timu hiyo ndiyo iliyoitoa Yanga kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2017/18 ambapo mechi ya kwanza iliyochezwa uwanja wa Taifa, Yanga walifungwa bao 2-1 wakati marudiano timu hizo zilitoka sare tasa.
Lengo la mechi hizo limewekwa kwaajili ya kocha Patrick Aussems kuangalia namna ambavyo anaweza kupata kikosi cha kwanza kwaajili ya msimu ujao.
Mpaka sasa kocha huyo anatengeneza timu na kuangalia mapungufu na uimara wa nyota wake baada ya timu hiyo kufanya usajili wa wachezaji 13 wapya.
Simba inajiandaa na michuano ya Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuanza Agosti 23 mwaka huu pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika ikiiwakilisha Tanzania baada ya kutwaa ubingwa wa ligi msimu uliopita.
Mratibu wa Simba, Abbas Seleman amesema; "Kambi inaendelea vizuri na tutacheza mechi tatu ambapo mechi mbili tunaendelea na mazungumzo na timu mbalimbali isipokuwa mechi ya Julai 27 ndiyo imethibitishwa kuwa tutacheza na Township Rollers,".