Waarabu wa Simba washangilia staili ya Makambo

Saturday January 12 2019

 

By ELIYA SOLOMON

MASHABIKI wa Simba SC,  wamejibu mapigo ya mashabiki wachache wa Yanga ambao wameungana na wa JS Saoura kwa kushangilia staili ya kubana mikono ya Makambo.

Mara kadhaa mashabiki hao wa Yanga ambao jezi zao zinafafana rangi na za Saoura walikuwa wakionekana wakishangilia kwa staili hiyo kabla ya Simba kupata mabao.

Mashabiki hao wachache ni kama walinyamazishwa na bao la Mganda Emmanuel Okwi mwishoni mwa kipindi cha kwanza.

Bao la Kagere ambaye aliingia kuchukua nafasi ya John Bocco aliyeumia liliwafanya mashabiki wa Simba kujibu mapigo kwa kushangilia kwa kubana mikono.

Washabiki hao wakiwa na furaha walikuwa wakibana mikono hiyo huku wakiwaangalia mashabiki wa Yanga na Saoura ambao walinyamazishwa na bao hilo la Kagere.

Advertisement