Vyakula hivi husaidia ngozi kuwa laini

Muktasari:

  • Watu wanahakikisha muda wote wanakuwa na sura au ngozi mwororo zenye mvuto, zisizoonyesha dalili za kuchujuka.

TUNAISHI katika karne ambayo kila mmoja hasa wakazi wa mijini, wakubwa kwa watoto anawaza kuwa katika ubora wa hali ya juu katika muonekano wake.

Watu wanahakikisha muda wote wanakuwa na sura au ngozi mwororo zenye mvuto, zisizoonyesha dalili za kuchujuka.

 Hii ndio imekuwa ishu kubwa kwa watu wengi kujitahidi kuhakikisha ngozi zao hazichujuki haraka kadri umri unavyokwenda.

 Mjini wapo waliozamia aina mbalimbali ya mafuta ziliotengenezwa kwa ajili ya kumpunguzia mtu kasi ya kuzeeka. Wapo wale waliokimbilia plastic surgery kudumisha mwonekano wa mtu mchanga.

 Kile baadhi yao walichosahau ni kwamba kuna aina ya vyakula ambavyo mtu akifanya mazoea ya kuvila, navyo kwa asilimia kubwa husaidia kupunguza kasi ya ngozi ya mtu kuchujuka hivyo kuzeeka kadri umri wake unavyokwenda.

Kwa utafiti uliofanywa na kuchapishwa na jarida la Healthline zifuatazo ndizo vyakula bomba vitakavyokuhakikisha ngozi mwororo kwa miaka mingi.

WATERCRESS

 Ni aina fulani ya mboga za majani inayopatikana Ulaya na  Bara la Asia. Huwa na wingi wa madini ya calcium, potassium, manganese, phosphorus na vitamin A,C,K, B-1 na B-2

 Majani haya husaidia katika kuongeza kasi ya usambasaji wa madini kwenye seli za mwilini. Kwa kufanya hivyo, huhakikisha ngozi inapata oxjeni ya kutosha hivyo kung’aa. Lakini hata zaidi, wingi wake wa madini ya vitamin A na C husaidia ngozi kupambana na miale hatari ya jua, hivyo kusaidia ngozi kutopata makunyanzi. Inashauriwa kuliwa kama saladi.

RED BELL PEPPER

Ni aina ya pilipili iliyopo kwenye familia moja na pilipili hoho. Huwa na wingi wa madini ya antioxidant (Carotenoids) ambayo ni muhimu sana katika kuondoa uchafu kwenye seli za mwili.

 Carotenoids ndio huchangia mimea mbalimbali kuwa na rangi hasa matunda na mboga. Carotenoids husaidia pakubwa ngozi kupambana na athari za miale mikali ya jua.

PAPAYA

 Tunda hili huwa na wingi wa antioxidants, vitamin na madini mengine ambayo ni muhimu kwenye maboresho ya ngozi.

 Madini yake hasa papain husaidia pakubwa kupambana na uwezekano wa ngozi kupata makunyazi hivyo kuhakikisha ni laini muda wote hivyo mazoea ya kuila hupunguza kasi ya ngozi kuchujuka licha ya umri kuzidi kusonga.

BLUEBERRIES

 NI miongoni mwa matunda kwneye familia kubwa ya berries. Huwa na wingi wa madini ya vitamin A & C na vile vile antioxidant anthocyanin ifahamikayo kwa kupambana na uzee.

 Madini yapatikanayo kwenye tunda hili husaidia mwili kupambana na presha ya miale ya jua, stresi na uchafuzi wa mazingira unaoweza kuathiri ngozi.

BROCCOLI

 Ni aina ya mboga ambayo hupatikana kwenye hoteli kubwa kubwa. Huwa na wingi wa vitamin C ambayo huchangia pakubwa utengenezaji wa protini ain ya Collagen mwilini.

 Collagen ndio huipa ngozi udhabiti wake na uwezo wa kupambana na kupasuka au kukunjana.

SPINACH

 Ni aina ya mboga ambayo madini yake kazi kubwa huwa ni kuongeza kasi ya seli za mwili kupata Oxygen ya kutosha na katika hilo kusaidia ngozi kung’aa. UKiachia mbali wingi wake wa Vitamini C ambayo ni muhimu sana kwenye utengenezaji wa protini ya Collagen, pia ina madini ya vitamin K ambayo husaidia kuzipa nywele udhabiti na mwenekano wa kung’aa

NJUGU

 Zipo aina nyingi tu za mbegu hii. Hata hivyo nyingi yazo hasa Almonds, huwa na wingi wa vitamin E ambayo husaidia pakubwa katika urekebishaji wa tishu za ngozi pale zinapochujuka, kudumisha hali ya ulaini wa ngozi na vile vile kulinda ngozi dhidi ya miale hatari ya jua.

AVOCADO

 Ni tund ambalo huwa na wingi wa mafuta muhimu mwilini. Mafuta haya husaidia kwenye kupromoti ngozi nyororo muda wote.

 Pia husaidia kwenye uondoaji wa seli nzee za ngozi na kuzipa zile mpya fursa za kuwa bora.

VIAZI VITAMU

 Huwa na madini ya antioxidant (beta-carotene) ambayo hubadilishwa mwilini na kuwa Vitamini A ambayo husaidia kuipa ngozi uwezo wa kujipinda kwa urahisi bila ya kusababisha makunyanzi na pia kuifanya kuwa nyororo. Pia ina Vitamini C na E ambazo huzuia madhara ya miale ya jua na kuifanya ngozi kung’aa.

MBEGU ZA POMEGRANATE

 Kwa miaka mingi zimetumika imetumika kama tunda lenye manufaa ya dawa. Huwa na wingi wa Vitamin C.