Viongozi Simba watua Uwanja wa Amaan

Sunday January 6 2019

 

By Mwanahiba Richard

Viongozi wa Simba wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Cresentus Magori wamewasili visiwani Unguja leo hii kwa ajili ya mambo makuu mawili.
Magori ameongozana na viongozi wenzake ambao ni Mwenyekiti Swedy Mkwabi, wajumbe wa bodi Salum Abdallah 'Try Again' na Zawadi Ally.
Kabla ya kushuhudia mechi yao na KMKM viongozi hao walifanya kikao na benchi la ufundi pamoja na kuzungumza na wachezaji.
Jambo la pili ni kuwapa morali wachezaji wao ambapo viongozi wote wanne wanashuhudia mechi hiyo inayoendelea uwanja wa Amaan ambayo ni ya hatua ya makundi.

Advertisement