Vinicius humwambii kitu kwa Kim Kardashian

Muktasari:

Akijibu maswali ya mashabiki katika chaneli yake ya YouTube, Vinicius Jr alipoulizwa ni staa gani angependa kutoka naye kimapenzi aliitaja familia ya Kardashian ambayo Kim ni mmoja wao. Mbali na swali hilo kuna shabiki mwengine alitaka kujua kati yake na Luka Modric nani mbaya sana?

MADRID, HISPANIA . UKIMWAMBIA kinda wa Real Madrid, Vinicius Junior achague demu unajua atamchagua nani? Fasta tu jina la Kim Kardashian ndilo litatoka kwenye kinywa chake.

Unajua kwa nini? Vinicius mwenyewe amefunguka kuwa anawakubali sana warembo wa familia ya Kardashian, ambayo mbali na Kim ina walimbwende kama Kourtney, Khloe, Kendall Jenner na Kylie.

Akijibu maswali ya mashabiki katika chaneli yake ya YouTube, Vinicius Jr alipoulizwa ni staa gani angependa kutoka naye kimapenzi aliitaja familia ya Kardashian ambayo Kim ni mmoja wao. Mbali na swali hilo kuna shabiki mwengine alitaka kujua kati yake na Luka Modric nani mbaya sana?

Staa huyo alijibu swali hilo kwa kusema anamheshimu sana Modric kwa hivyo hawezi kutoa jibu la swali hilo. Kuhusiana na beki gani mgumu ambaye amewahi kukutana naye mwenyewe aliwataja mabeki wa Real Madrid, Eder Militao na Sergio Ramos ambao alidai huwa wanampa wakati mgumu sana wakiwa kwenye uwanja wa mazoezi. Kuna shabiki alitaka kujua kama kinda huyo amewahi kufanya mapenzi, lakini Vinicius aliishia kumshangaa mtu aliyeulizwa swali hilo kwa kumuliza kama alimaanisha alichouliza.