Vigogo Ligi Kuu Kenya hoi

Tuesday March 19 2019

 

By Vicent Opiyo

VIGOGO wa Ligi Kuu ya KPL waliangushwa wikiendi kwenye mechi za ufunguzi za raundi ya 32 za michuano ya Ngao ya SportPesa.

Sofapaka, iliyopoteza fainali ya mwaka jana baina ya Kariobangi Sharks, ilibanduliwa nje na limbukeni Bungoma SuperStars 5-4 matuta baada ya sare tasa muda wa kawaida. Nayo Ulinzi Stars, iliopoteza fainali ya mwaka 2016 kwa Tusker, ikaondolewa na SS Assad 5-4 kwa penalti pia baada ya mechi kuishia sare ya kutofungana.

Ushuru pia ilipigwa 2-0 na Vihiga Sportiff huku mabingwa watetezi Sharks wakianza kampeni ya kuhifadhi taji lao kwa kuwanyuka Elim FC 5-0 ugani Bukhungu.

Mabingwa mara 10 AFC Leopards waliwanyeshea Transfoc ya Kitale 4-0 na kufuzu raundi ya 16 bora. Gor Mahia itachuana na Kenpoly hapo kesho kwenye mechi yao ya raundi ya kwanza.

Timu za KPL Western Stima, Bandari, KCB, ni nyingine zilizofuzu.

baadhi ya MATOKEO YA WIKIENDI

Uprising 0-5 Western Stima (Ruaraka Grounds)

Congo Boys 2(3)-2(2) Kenya Police (Serani Sp.Grounds)

SS Assad 0(5)-0(4) Ulinzi Stars (Ukunda Grounds)

Bungoma Superstars 0(5)-0(4) Sofapaka (Sudi Stadium)

Muranga Seal 4-1 Kisumu All Stars (Kiharu Stadium)

Transmara Sugar vs Bidco United (Gusii Stadium).

 

Advertisement