Vigogo Gor Mahia kuchunguzwa, kisa kushindwa kufuzu Afcon

Muktasari:

  • Mkurugenzi wa Ufundi wa Admiral Youth FC, Aref Baghazally aliomba kuchaguliwe kamati maalum ya kuchunguza kile kilichoifanya timu hiyo kufanya mambo ya aibu hasa kuwafanya wachezaji wake kulala kwenye uwanja wa ndege.

MOMBASA .UCHUNGUZI unatakiwa kufanyika juu ya sakata ya Gor Mahia ambayo ilisababisha kushindwa kufuzu kwa nusu fainali ya mashindano ya Kombe la Mashirikisho baada ya kushindwa vibaya na klabu ya Morocco.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Admiral Youth FC, Aref Baghazally aliomba kuchaguliwe kamati maalum ya kuchunguza kile kilichoifanya timu hiyo kufanya mambo ya aibu hasa kuwafanya wachezaji wake kulala kwenye uwanja wa ndege.

“Gor Mahia walikuwa wawakilkishi wan chi yetu ya Kenya na hivyo waliwajibika wachezaji wafanyiwe mambo mazuri ili waweze kufanya vizuri kwenye mechi zao. Lilotokea kwenye safari yao ya kwenda Morocco lilikuwa la aibu na kuiziri nchi yetu,” akasema Baghazally.

Alisema inashangaza kwa klabu ambayo ilifika robo fainali ya mashindano hayo ambayo pesa zinaingia kwa klabu, iwe inashindwa kuwahudumia wanasoka wao vizuri ikli waweze kupata matokeo mazuri ya ushindi,

“Ni muhimu kwa Wakenya kutambua sababu hasa ya timu hiyo kushindwa kufanya vizuri kwani katika mechi zao za mwanzo, timu ilkifanya vizuri sana n ahata tulikuwa na tamaa tutaweza kufuzu hadi fainali n ahata kuchukua kombe,” akasema mkurugenzi huyo.

Aliomba serikali iwe ikijitolea na kuweka hazina maalum ya kuwezesha pesa kutoka kwa haraka ili timu zetu zinazokwenda ugenini kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa, iweze kupata huduma za haraka.