VIDEO: Stars yatua Cameroon kwa muda

Muktasari:

  • Miongoni mwa vigogo waliosafiri ni Kaimu Rais wa TFF, Athuman Nyamlani, wajumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho hilo, Francis Ndulane na Lameck Nyambaya, Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah 'Try Again', katibu mkuu wa zamani wa TFF, Angetile Osiah, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Shani Chrisostoms.

Msafara wa watu 85 wa timu ya Taifa 'Taifa Stars', umetua Cameroon saa nne asubuhi ya leo kwa mapumziko mafupi kabla ya kuelekea Cape Verde itakapotua jioni ya leo.

Msafara huo ulioondoka leo saa 9.00 Alfajiri, utasimama Cameroon kwa muda ili kujaza ndege mafuta kisha kuelekea Praia ukiongozwa na Mkurugenzi wa michezo Tanzania, Yusuph Singu.

Katika kundi hilo la watu 85, jumla ya wachezaji 26 wamesafiri wakiwemo nyota watano wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi.

Wachezaji hao 26 wataungana na wengine wanne, Mbwana Samatta, Saimon Msuva, Farid Musa na Shaban Iddi ambao wataungana na timu Cape Verde.

Stars imesafiri na kundi kubwa la vigogo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), wadau pamoja na waandishi wa habari za michezo.

"Nadhani mnafahamu kuwa Tanzania haijashiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa muda mrefu hivyo tuna imani mtakwenda kupambana na mtapata ushindi.

Serikali iko pamoja na nyinyi katika kila hatua na tuna imani mtapeperusha vyema bendera ya nchi yetu," alisema Dokta Mwakyembe.