VIDEO: Simba yaiduwaza Al Ahly, ikishinda bao 1-0 Taifa

Muktasari:

Bao pekee la Simba liliwekwa wavuni na Meddie Kagere dakika ya 64 na kuwafanya mashabiki kulipuka kwa shangwe uwanjani hapo.

Timu ya Simba imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Kundi D leo Jumanne.

Bao pekee la Simba liliwekwa wavuni na Meddie Kagere dakika ya 64 na kuwafanya mashabiki kulipuka kwa shangwe uwanjani hapo.

Awali, Kipindi cha kwanza kilimalizika katika bila kufungana huku mchezo huo ukionekana kuwa mgumu kwa kila timu.

 Simba ambao katika mechi ya kwanza dhidi ya wapinzani wao nchini Misri walikubali kufungwa mabao 5-0 lakini katika mechi hii Simba wakiwa nyumbani walionekana kuimarika tofauti na mechi iliyopita ambapo kipindi cha kwanza tu walikuwa wameshakula tano.

 Simba walishindwa kupata mabao a mapema licha ya kupata nafasi tatu kipindi cha kwanza ambazo kama wangeongeza umakini walikuwa na uwezo wa kufunga.

Nafasi ya kwanza ilikuwa dakika 9, Emmanuel Okwi aliwapiga chenga mbeki wa Al Ahly na kupiga shuti ambalo lilinyakwa na kipa.

Maddie Kagere alipata pasi nzuri mbili dakika ya 12, ambapo alishindana na walinzi wa Al Ahly ambapo alipata nafasi na kupiga shuti  lililopanguliwa na kipa na kuwa kona.

 Kagere alifanya hivyo tena dakika 40, baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Chama na kupiga shuti ambalo lilipanguliwa na kipa na kuwa kona tena.

Simba walifanya mabadiliko dakika 39, kwa kumtoa Asante Kwasi na kuingia nahodha msaidizi Mohamned Hessein 'Tshabalala'. Al Ahly wao walifanya mashambulizi ya kushtukiza lakini muda mwingi walikuwa chini ya ulinzi wa Simba.

Baadaye nafasi ya John Bocco ilichukuliwa na Hassan Dilunga kipindi cha pili.

Kama Simba wangeweza kuongeza umakini katika nafasi walizopata hasa mastraika wote wawili Okwi na Kagere wangeweza kumaliza kipindi cha kwanza wakiwa mbele.