VIDEO: Shabiki Geita Copa Umisseta aomba usajili Yanga

Friday June 8 2018

 

By Imani Makongoro

Mwanza. Mashabiki wa mkoa wa Geita hata timu yao ya Copa Umisseta kifungwa wao hawapoi kabisa kushangilia, kumbe bwana jamaa wako njiani kwenda Yanga.


Geita wanastaili yao ya ushangiliaji katika mashindano hayo ambapo mashabiki wake kwanza wameibuka na vazi la chupa za plastiki, kupaka chokaa usoni na kofia za asili kichwani na haijalishi kama wamefungwa au wanafungwa wao ni kushangilia mwanzi mwisho.


"Tunatamani sana kujiunga na kundi la ushangiliaji la Yanga, tulikuwa tunapenda staili ya ushangiliaji ya Ally Yanga (Marehemu) lakini huku tuliko kupata masizi ni kazi hivyo tunatumia chokaa," alisema Kabayonga Joseph.


Timu ya Geita imesafiri na Kabayonga na Richard Robert ambao kazi yao ni moja tu kuzishangilia timu za mkoa huo na katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na kampuni ya Coca Cola Tanzania, mashabiki hao wamefunika kwa staili yao ya ushangiliaji.

Advertisement