VIDEO: Seseme kuikosa Yanga

Muktasari:

  • Seseme ni miongoni mwa nyota wa kikosi cha Mwadui Fc, kukosekana kwake kulizua hofu kwa upande wa mashabiki wa timu hiyo yenye maskani yake Shinyanga.

Dar es Salaam. Kiungo Abdallah Seseme wa Mwadui ataukosa mchezo leo dhidi ya Yanga baada ya kuachwa mkoani Shinyanga kutokana na kupata majeraha.

Kocha wa Mwadui, Ally Bizimungu alisema amemuacha nyota huyo ili kupona majeraha yake aliyoyapata katika mechi zilizopita.

“Seseme ni mchezaji mzuri, lakini haipendezi nikamfosi acheze huku akiwa hajapona vizuri, nimeona bora abaki afanye mazoezi katika program nilizomuachia ili mpaka tukirudi atakuwa fiti,” alisema Bizimungu.

Akizungumzia kuhusu pengo la mchezaji huyo katika mchezo wao dhidi ya Yanga, alisema ameshatafuta njia mbadala muda mrefu kuhakikisha jambo hilo halionekani.

“Seseme hakuumia jana wala juzi kwahiyo kuna watu walikuwa wanacheza eneo lile, hata alivyopona alirudi na kucheza lakini hakuwa yule yule kwahiyo njia pekee ya kumfanya arejee katika kiwango chake ni kupona kabisa,” alisema.

Mwadui itakuwa na kibarua kigumu leo saa moja usiku itakapocheza na Yanga katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.