VIDEO: Ronaldo arejea mazoezini Juventus

Tuesday May 19 2020

 

By AFP

Turin, Italia. Cristiano Ronaldo amerejea mazoezini katika klabu yake ya Juventus leo jijini Turin baada ya kutofanya mazoezi kwa takriban miezio miwili kutokana na ugonjwa wa virusi vya corona, Covid-19.


Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35 aliwasili Kituo cha Mazoezi cha Juventus akiendesha gari aina ya Jeep ambalo vioo vyake vimewekwa tint.


Mshindi huyo wa tuzo tano za Mwanasoka Bora wa Dunia atalazimika kufanyiwa uchunguzi wa afya na utimamu wa mwili kabla ya kujiunga na wenzake mazoezini, kw amujibu wa taarifa za vyombo vya habari.


Wachezaji wa Juventus waliwasili kwa ajili ya mazoezi ya mmojammoja Mei 4, siku ambayo Ronaldo alirejea Italia baada ya kutoka Ureno ambako kulikuwa na amri ya kuzuia kutoka.


Kwa wiki mbili zilizopita, Ronaldo alikaa karantini katika jumba lake la jijini Turin.


Ronaldo aliicheza wakati Juventus ilipocheza mechi ya mwisho ya Ligi Kuu ya soka ya Italia, Serie A, kabla haijasimamishwa, na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Inter Milan. Mechi hiyo ilichezwa bila ya mashabiki katika uwanja wa  Allianz Machi 8.

Advertisement


Italia ni moja ya nchizilizoathiriwa sana na Covid-19, ikipoteza zaidi ya watu 32,000.
Juventus iko juu ya Lazio kw atofauti ya pointi moja wakati ikisaka ubingwa wa Italia kwa mara ya tisa mfululizo.


Ronaldo ini mchezaji wa kwanza wa kigeni katika klabu ya Juventus kati ya walioondoka Italia wakati wa mlipuko wa virusi vya corona, kurejea katika kituo cha mazoezi cha Continassa.
Shirikisho la Soka la Italia (FIGC) lilitangaza jana kuwa mashindano yake yote, ikiwemo Serie A, yataendelea kusimama hadi Juni 4.
   

Advertisement