VIDEO: Kampeni za uchaguzi Yanga kumekucha!

Muktasari:

Mchungahela alisema uchaguzi huo unatarajiwa kuwa wa amani huku wagombea wote wakiwa na haki ya kupiga kampeni katika matawi yao.

KAMPENI za uchaguzi wa klabu ya Yanga zimezinduliwa leo rasmi na Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi TFF, Ally Mchungahela, huku akitaka uchaguzi huo kufanyika kwa amani.
Mchungahela alisema uchaguzi huo unatarajiwa kuwa wa amani huku wagombea wote wakiwa na haki ya kupiga kampeni katika matawi yao.
"Tawi ni mali ya klabu hivyo mgombea yoyote anaruhususiwa kwenda kufanya kampeni yake, kama hutaki kumsikiliza unaweza ukaondoka na kuachana nae," alisema.
Akizungumzia kuhusu wanachama wanaotakiwa kupiga kura, alilisisitiza ni kwa wanachama wote ambao wana kadi za uanachama wa Yanga.
"kadi zote iwe ya kitabu au hizi mpya unaruhusiwa kupiga kura, kwahiyo wanachama watambue hilo na kwa wale mashabiki ambao sio wanachama wawe watulivu kusubili matokeo," alisema.
Wakati huo huo mjumbe wa kamati ya Utendaji Yanga, Siza Lyimo alisema kwamba wanachama wanatakiwa walipie kadi zao ili waweze kupiga kura.
Uchaguzi wa Yanga  wa kujaza nafasi zilizowazi unatarajiwa kufanyika tarehe 13 katika ukumbi wa Osyterbay jijini Dar es Salaam.