VIDEO: Cannavaro atua Moro aanza kazi

Thursday August 9 2018

 

By Khatimu Naheka

Morogoro. Meneja mpya wa Yanga, Nadir Haroub Cannavaro amewasili kambini tayari kwa kuanza majukumu yake mapya.

Mkongwe huyo aliyestaafu msimu huu ametua kambini Yanga jana usiku na asubuhi hii alikuwepo mazoezini.

Cannavaro amesema kwasasa yuko tayari kwa majukumu yake hayo baada ya kustaafu soka.

Alisema ameridhishwa na maandalizi aliyoyaona ikiwemo kambi yao na kwamba makocha wanafanya kazi kubwa kuitengeneza timu yao.

Aliongeza alisema hata wachezaji wao nao wako sawa na kwamba Wanayanga wamuunge mkono katika jukumu lake hilo.

Advertisement