Utalii wamkumbuka Ruge Mutahaba

Muktasari:

  • Ruge Mutahaba alifariki nchini Afrika Kusini mnamo Februari 26, 2019 alikokuwa akipatiwa matibabu ya figo.
  • Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zenye vivutio vya kitalii.

Dar es Salaam. Aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi wa Clouds, Ruge Mtahaba ametajwa wakati wa uzinduzi wa video ya kuhamasisha utalii wa Tanzania duniani.
Ruge ambaye alifariki mwaka jana ametajwa na Waziri wa Mali Asili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla kuwa miongoni mwa wanakamati walioshiriki kuandaa video hiyo hiyo iliyopewa jina la Tanzania Unforgettable (Tanzania haisahauliki).
"Tulikuwa na Ruge kwenye harakati zote za maandalizi ya video hii, hadi imekamilika na leo imezinduliwa," alisema Dk Kigwangalla.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya utalii Tanzania (TTB), Devotha Mdachi amesema video hiyo imetengenezwa nchini na iko kwa lugha mbalimbali ikiwamo kingereza, kichina, kiisrael na lugha nyingine nyingi.
Amesema video hiyo itasambazwa kwenye balozi mbalimbali za Tanzania duniani ili kuwapa fursa watu wa mataifa hayo kuishuhudia.
"Imeonyesha vivutio vyetu vingi vya utalii, tunaamini itasaidia kuongeza watalii nchini," amesema.