Fundi wa Stand United njia nyeupe Majimaji

Wednesday December 6 2017

 

Beki wa Stand United 'Chama la Wana', Hamad Kibopile, yupo mbioni kujiunga na Majimaji ya Songea, kupitia usajili wa dirisha dogo.
Kibopile aliyewahi kucheza Mbeya City alisema; "Kazi yangu ni kucheza ikifika wakati mwafaka kila jambo linakuwa wazi, kwa sasa siwezi kuzungumzia chochote juu ya hilo,"alisema.
Kabopile ambaye anasifika kwa mipira ya kurusha ambayo huwa kama kona, alisisitiza kuwa zipo timu nyingi zilizomfuata kutaka huduma yake, lakini anapenda kuzingatia sheria na siyo kwenda kihuni.
Aidha, Chama la Wana limepokea nyota wawili kwa mkopo Frank Zakaria na Mohammed Titi kutoka Singida United ambayo pia imeachana na nyota wengine wawili Atupele Green aliyeomba kuondoka kikosini na Pastory Athanas.