Usaili Miss Utalii wanarudi upyaaaa

Friday August 2 2019

 

By Rhobi Chacha

INARUDI tena. Ndio, baada ya kupita miaka 6 bila kufanyika kwa Shindano la Urembo la Miss Utalii, goma limerudi upyaaa.

Shindano hilo lilisitishwa mwaka 2013, linatarajia kurudi kwa kishindo mwishoni mwa mwezi huu likiwa limeboreshwa.

Mratibu wa shindano hilo, Gideon Chipungahelo ‘Chips’ amesema tayari maandalizi yameanza na kwamba usaili wa kuwapata warembo utafanyika katika kanda saba ambazo ni Kaskazini, Swahili Coast, Mashariki, Magharibi, Nyanda za Juu Kusini,  Kanda ya Ziwa na Kati.

“Shindano hili litakuwa na nguzo kuu mbili ambazo ni Kanda na Taifa, tutaanza usaili mwishoni mwa mwezi huu, tumeunganisha mikoa kulingana na kanda zilivyo," alisema Chips

Aidha Chips amesema, Basata walilifungia shindano hilo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutakiwa kuendeshwa kama taasisi na si mtu mmoja kama ilivyokuwa ikifanyika.

Na hilo amesharekebisha na kwamba mambo ndio yameanza na kuwataka wadau wa shindano hilo kujiandaa kupata burudani waliyoikosa kwa muda mrefu.

Advertisement

Shindano hilo ambalo lililenga kutangaza utalii wa ndani nan kuipaisha Tanzania lilifungiwa baada ya baadhi ya mambo kuonekana hayapo sawa kama njia ya kuwanyoosha wahusika uli warudi kivingine.

 

Advertisement