United yamtaka Eriksen kwa bei chee Januari

Muktasari:

Mbali na Inter Milan ambayo inamtaka lakini Real Madrid inaweza kuibuka na kuweka dau la kumnchukua kama bado itashindwa kumnasa kiungo wa Man United, Paulo Pogba ambaye amebaki Old Trafford bila ya kutegemewa.

MANCHESTER United inaamini itaweza kumnasa kiungo mahiri wa Tottenham, Christian Eriksen, 27 katika dirisha la Januari kwa bei kiduchu baada ya kuingia mwaka wa mwisho wa mkataba na klabu yake ya London.

Eriksen atakuwa amebakiza miezi sita tu ifikapo Januari mwakani na dau lake litakuwa chini na Manchester United inaamini kwamba Tottenham inaweza kulazimika kumuuza staa huyo wa kimataifa wa Denmark kwa ajili ya kuhofia asiondoke bure.

Hata hivyo, United itakumbana na upinzani kutoka kwa Inter Milan ambayo pia inamtaka staa huyo na kwa mujibu wa kanuni Eriksen anaweza kusaini mkataba katika klabu ya nje ya England ifikapo dirisha la Januari.