United, Inter zatangulia robo fainali Europa

Muktasari:

Manchester United imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali baada ya kuibamiza LASK ya Australia mabao 2-1, huku matokeo ya jumla yakiwa ni 7-1, baada ya United kufanikiwa kushinda 5-0 katika mchezo wa awali.

MANCHESTER, ENGLAND

Mshike mshike wa hatua ya 16, katika michuano ya Europa League umeendelea jana kwa michezo minne kupigwa.

Manchester United ikiwa nyumbani katika Uwanja wa Old Trafford imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali baada ya kuibamiza LASK ya Australia mabao 2-1, huku matokeo ya jumla yakiwa ni 7-1, baada ya United kufanikiwa kushinda  5-0 katika mchezo wa awali.

Mabao ya United yalifungwa na Jesse Lingard dakika ya 57, akisawazisha bao la LASK ambayo ndio ilianza kutangulia kwa bao lilifungwa na    Philipp Wiesinger dakika ya 55 huku bao la pili na la ushindi kwa United likafungwa na Antony Martial dakika ya 88.

Mchezo mwingine ulikuwa kati ya Inter Milan iliyokuwa nyumbani dhidi ya Getafe ambapo Inter ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali.

Miamba ya Ujerumani Wolfsburg ikafurushwa nje ya michuano hiyo baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Shakhtar Donetsk na matokeo ya jumla yakawa ni 5-1, baada ya mchezo wa kwanza wa kumalizika kwa Shakhtar kushinda mabao 2-1.

FC Koebenhavn ikiwa nyumbani ikapindua meza kibabe baada ya kuichabanga istanbul Basaksehir mabao 3-0, na matokeo ya jumla kusoma 3-1, kwa kuwa mchezo wa kwanza FC Koebenhavn kupigwa bao 1-0.

 

Mechi za leo

Bayer Leverkusen vs Rangers (1:55 usiku)

Sevilla vs Roma (saa1:55 usiku)

 

FC Basel vs Intracht Frankfurt (4:00 usiku)

Wolverhampton Wanderers vs Olympiacos (4:00 usiku)