Umeisikia hii? Mke wa Yondani afanya kufuru Dar

Muktasari:

Kelvin Yondani 'Vidic' na mkewe Nance Mussa wamekuwa pamoja kwa zaidi ya miaka 10, na mwaka jana ndiyo walifunga ndoa rasmi.  

Dar es Salaam. Mke wa beki na nahodha wa Yanga, Kelvin Yondani 'Vidic' anayeitwa Nance Mussa amefanya 'kufuru' katika sherehe za usiku wa zawadi harusi ya Mrundi Amissi Tambwe.

Mrembo huyo mwenye watoto wawatu aliozaa na Yondani, alifanya tukio hilo wakati wa ugawaji wa zawadi ambapo mbali na kutoa ya jumla, yeye mwenyewe aliamua kutoa ya kwake.

Hapo ndipo akafanya mambo ambapo alitunza noti za elfu kumi kumi huku akisindikizwa na wimbo na baada ya MCL Digital kufuatilia zilikuwa shilingi laki moja.

Amesema, aliamua kufanya hivyo kwa sababu ya ukaribu wake na mke wa Tambwe anayeitwa Raiyan.

Sherehe hizo zilifanyika kwenye Ukumbi wa CCM Ilala Boma jijini Dar es Salaam.