Ukame wa mabao Man City wamtia presha Guardiola

Muktasari:

Man City inaongoza katika Kundi A ikiwa na pointi sita baada ya kushinda mechi mbili na leo itacheza na kibonde Atalanta ikiwa nyumbani Uwanja wa Etihad.

London, England. Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amekata tamaa ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.

Kocha Pep alisema matumaini ya Manchester City kutwaa ubingwa hakuna kwa sababu hana kikosi imara cha ushindani.

Alisema licha ya kufanya usajili wa Pauni580 milioni, lakini ndoto yake ya kutwaa ubingwa imefifia.

“Watu wanazungumzia kuhusu ubingwa wa Ulaya. Hatuko tayari kwa hilo, tumetengeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini hatukufunga, tunahitaji kuongeza kasi,” alisema Guardiola.

Kocha huyo alisema misimu miwili iliyopita wafunga idadi kubwa ya mabao, lakini msimu huu hali imekuwa tofauti.

Man City inaongoza katika Kundi A ikiwa na pointi sita baada ya kushinda mechi mbili na leo itacheza na kibonde Atalanta ikiwa nyumbani Uwanja wa Etihad.

Kocha huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich, alisema bila wachezaji wake kubadilika, Man City haitakuwa na ubavu wa kutwaa ubingwa.