Ujio wa kocha washtua mashabiki wa Gor Mahia

Muktasari:

  • Hatua ya uwepo wake umeishia kuzua uvumi kwamba yupo nchini kuchukua nafasi yake kocha wa Gor, Hassan Oktay

HIVI unamkumbuka kocha wa zamani wa Gor Mahia na watani wao AFC Leopards Mcroatia Zdravko Logarusic?

Kocha huyo aliyeishia kupata umaarufu mkubwa hapa nchini  alitua nchini na kuonekana kwenye mechi ya Gor  na Hussein Dey ambapo alisalimiana na mashabiki.

Hatua ya uwepo wake umeishia kuzua uvumi kwamba yupo nchini kuchukua nafasi yake kocha wa Gor, Hassan Oktay ambaye  inasemekana anafukuziwa na Wamisiri Zamalek na vile vile Petro Atletico wa Angola.

Oktay alikiongoza kikosi chake kuwalima Zamalek magoli 4-2  uwanjani Kasarani kabla ya kusafiri hadi Angola walikolimwa  na Petro 2-1.

Hata hivyo uwezo wake wa kupanga kikosi na ufundi wake umeonekana kuzivutia klabu hizo mbili ambazo sasa zinasemekana zimekuwa zikimfukuzia kimya kimya.

Taarifa hizo zilishawafikia viongozi wa Gor na kwa haraka sana wakamua kumvuta Loga kuchukua nafasi yake kama akiamua kuondoka.

Hata hivyo Logarusic kafutilia mbali tetesi hizo kwa kusema hajaja Kenya kuridhi mikoba ya kocha yeyote akisisitiza kwamba amekuja kutembea.

“Nilipata fursa ya kwenda likizo fupi na nikaamua kuja Kenya kujivinjari  kwa sababu ni karibu na Sudan. Isitoshe hali ya anga huku ni bora zaidi ikilinganishwa na Sudan ambapo joto ni kali sana. Pia chakula ni kizuri huku” Loga akafunguka.

Licha Loga  bado  ni kocha wa timu ya taifa ya Sudan, amesema  hawezi kuipiga chini ofa ya kuinoa tena klabu ya KPL kama ikitokea.