Ugonjwa wakwamisha kesi ya vigogo Simba

Dar es salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo  imeshindwa kuendelea na kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili waliokuwa vigogo wa klabu ya Simba kutokana na mshtakiwa wa kwanza Evans Aveva kuwa mgonjwa.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi ni aliyekuw Makamu wa  wake,  Geofrey Nyange maarufu (Kaburu) na Mwenyekiti wa  Kamati ya Usajili wa Klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe.

Wakili wa serikali Sylivia Mitanto alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba  kuwa Kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa lakini mshtakiwa wa kwanza hayupo.

Hakimu Simba alieleza kuwa amewasiliana na Wakili wa Takukuru Leonard Swai anaeendesha kesi hiyo nakumweleza yuko kwenye kikao hadi Mei 28 laki pia anayo taarifa ya mshtakiwa wa kwanza ambaye ni Mgonjwa.

Baada ya kueleza hayo Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 31 mwaka huu.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 10 ikiwemo kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi,  kutoa maelezo ya uongo na utakatishaji wa fedha.

Katika shitaka la utakatishaji fedha linalomkabili Aveva, inadaiwa Machi 15, 2016 katika benki ya Baclays Mikocheni, Dar es Salaam alijipatia Dola za Kimarekani 187,817, takriban Sh. Milioni 400 kutoka katika Timu ya Simba wakati akijua zimetokana na zao la kosa la kughushi.

Katika shitaka la kughushi linawakabili washtakiwa wote, ambapo wanadaiwa katika tarehe hizo hizo kwa pamoja walighushi hati ya malipo ya kibiashara ya Mei 28, 2016 wakionyesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zinathamani ya dola 40,577 sawa na zaidi ya Sh. Milioni 90 huku wakijua kwamba sio kweli.

Pia katika shtaka lingine inadaiwa Aveva, Nyange na Hans Poppe kati ya March10 na September 30, 2016 waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Kimarekani 40,577.