Uganda waanika kikosi cha awali

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tovuti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Uganda (FUFA), kikosi hicho kinaundwa na wachezaji Oyo Delton, Jack Komakech, Ssemwogerere Daniel, Sinalya Ben, Kevin Ssekimbegga, Ibrahim Juma, Kasozi Samson, Kizito Mugweri Gavin, John Rogers, Kiddawalime Saul, Wasswanga Shafik na Opira Innocent.


TIMU ya taifa ya Uganda chini ya umri wa miaka 17 ‘Uganda Cubs’ ambao ni wapinzani wa Tanzania ‘Serengeti Boys’ kwenye Fainali za Afrika kwa vijana wa umri huo, wametangaza kikosi cha wachezaji 30 kitakachoingia kambini kujiandaa na fainali hizo zitakazofanyika nchini kuanzia Aprili 14.

Kikosi hicho kitaanza kambi leo Jumanne kwenye kituo cha soka kilichopo Njeru nchini Uganda kabla ya kuelekea Uturuki kushiriki mashindano maalumu yanayoshirikisha nchi nane tofauti duniani, Serengeti Boys ikiwemo.

Ni ndani ya kundi hilo la wachezaji 30 watakalopatikana nyota 21 wataoshiriki fainali za Afrika ambazo Uganda wamepangwa kundi A pamoja na timu za Tanzania, Nigeria na Angola.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tovuti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Uganda (FUFA), kikosi hicho kinaundwa na wachezaji Oyo Delton, Jack Komakech, Ssemwogerere Daniel, Sinalya Ben, Kevin Ssekimbegga, Ibrahim Juma, Kasozi Samson, Kizito Mugweri Gavin, John Rogers, Kiddawalime Saul, Wasswanga Shafik na Opira Innocent.

Wengine ni Ekellot Ibrahim, Ssekajja Davis, Ziraba Ronnie, Kakaire Thomas, Mwaka Polycarp, Opaala Edwine Mukisa, John Kokas Alou, Mukisa Owen, Jarieko James, Asaba Ivan, Surundu Ibrahim, Najib Yiga na Yasin Abdu Owane.

Mbali na hao, wengine ni Mugulusi Isma, Lubega Derrick, Mugisha Rogers, Abdul Wahid Iddi na Kakande Shafic.