Uganda uso kwa uso na Angola

Muktasari:

Licha ya kocha huyo kuwa na uzoefu wa kutosha katika soka la Afrika, alisema rekodo yake haiwezi kucheza zaidi ya vijana wake kujituma.

KIKOSI cha timu ya Taifa Uganda chini ya miaka 17 kesho kinashuka uwanjani kukipiga na Angola mchezo ambao utakuwa wa pili katika ufunguzi wa Fainali za Afcon nchini.

  Kuelekea katika mchezo huo kocha mkuu wa Uganda, Samuel Kwasi alisema miundombinu iliyowekwa Uganda kwa vijana kunamfanya afanye kazi yake kiwepesi.

  "Hatuna cha kupoteza hapa kwasababu tuna Ligi nzuri ya vijana kiasi ambacho sipati tabu katika ufundishaji wangu, kumuelekeza mwanafunzi wa shule ni rahisi kuelewa," alisema.

   Licha ya kocha huyo kuwa na uzoefu wa kutosha katika soka la Afrika, alisema rekodo yake haiwezi kucheza zaidi ya vijana wake kujituma.

  "Mpira sio sawa na kusema moja jumlisha moja ni mbili ni kitu ambacho kipo uwanjani ni wachezaji wangu kujituma kwa nguvu zote na kuhakikisha tunafanya vizuri," alisema.

  Naye nahodha wa Uganda, Kizito Gavin alisema wamejiandaa kuja kufika hatua ya nusu fainali katika fainali hizi.  

  "Tumejiandaa kiakili na kimwili, tumekuja kuchukua pointi hapa na hii ni mara yetu ya pili hivyo tunahakikisha tunafika hatua ya nusu fainali,".