Ubutu wa washambuliaji wamnyima raha Minziro

Muktasari:

  • Safu ya ushambuliaji ya Arusha United kukosa mabao imeanza kumpa wasiwasi kocha mkuu wa kikosi hicho, Fred Minziro katika harakati zake za kupanda Ligi Kuu Bara na sasa anaifanyia kazi ili apate matokeo mazuri.

 

SAFU butu ya ushambuliaji kwenye kikosi cha Arusha united, umeanza kuleta shaka kwenye kikosi hicho kwenye matarajio yake ya kupanda Ligi Kuu msimu ujao.

Hali hiyo ilileta shaka kwenye mechi dhidi ya Boma FC ya Mbeya mchezo uliopigwa Mkoani hapa baada ya kupoteza nafasi zaidi ya tano ya kutikisa nyavu lakini zote hazikuzaa matunda hali iliyofanya Wana Utalii hao kugawana pointi kutokana na suluhu hiyo.

Mchezaji Ally kabunda dakika ya 21 Mara baada ya alifanikiwa kuwatoka wapinzani wao na kubaki na mlinda mlango pekee lakini alipaisha mnazi.

Dakika ya nyongeza 45, Hamad Kibopile naye alishindwa kuwanyanyua mashabiki wa timu hiyo alipopaisha mpira baada ya adhabu aliyopiga baada ya Ally Kabunda kuangushwa eneo la hatari.

Kocha mkuu wa kikosi cha Arusha united Fred Felix ‘Minziro’ alisema ubutu wa safu yake ya ushambuliaji anaitambua katika kikosi chake na imekuwa ikimnyima usingizi kutokana na makali anayowapa wachezaji wake lakini bado wanashindwa kufanya kazi ipasavyo.

“Safu ya beki ina afadhali, ingawa kuna wachezaji wakitengeneza pacha ina weka ukuta mzuri tatizo lipo kwa wafungaji ndio wananiangusha maana angekuwepo Zahoro Pazi aliyeumia mechi iliyopita angekuwa msaada kwa Jerry Katula na Ally Kabunda,

“Kocha wa Boma fc, Geofrey Katepa alisema kuwa kuvuna pointi moja ugenini ni faida kwao na wanaamini wataenda kujipanga kuhakikisha nyumbani hawapotezi chochote.