Ubishi mpya :Kwani Zari na mama Diamond nani mkubwa?

MTAANI ubishi ni mwingi sana. Wawakili wa ubishi wa mtaani, Luqman Maloto na Dk Levy wapo supa kukubishia wewe hapo msomaji.

LUQMAN: Oyoo Ogaa Levy. Vipi Amunike anaendeleaje huko, kashasepa zake?

LEVY: Asepe mara ngapi? Hivi tunavyoongea yuko kibarazani na mkewe huko wanapiga umbea tu wa Bongo.

LUQMAN: Si alikuwa anasuburi kuipeleka Taifa Stars Chan au ndio kubadili gia angani?

LEVY: Ashindwe na alegee. Nani anataka kufa kwa presha? Mtu mwenyewe utadhani anafundisha mgambo, muda wote timu inalinda goli kama Masai wa magetini?

LUQMAN: TFF imemtema Amunike, sasa atarudi kwao Nigeria au atabaki hapahapa alisongeshe Bongo Movie.

LEVY: Yaani hata kazi asipate. Asepe tu. Sawa tulizidiwa na timu za Kaskazini na Magharibi. Jamani ndo hata hawa kina Onyango? Ondieki Nyokakota na kina Mwala? Hao kina Omondi nao wametubagaza? Amunike akwende tu.

LUQMAN: Usiwe na liroho ligumu. Mwache tu apige kazi ili tufaidi unyama wa Kinigeria kwenye filamu za home. Mbona Patcho Mwamba alikuja kuimba muziki FM Academia, siku hizi ni staa Bongo Movie na mmemekubalia? Amunike ana kasoro gani?

LEVY: Patcho Mwamba tajiri alifanikiwa kwenye muziki. Ndo maana ikawa rahisi kupasua anga la Bongo Movie. Utambue tu Bongo Movie wana timu ya mpira.

LUQMAN: Hutaki Amunike awe kocha wa timu ya Bongo Movie?

LEVY: Sasa unadhani akienda kuigiza Bongo Movie atafanya kazi gani? ...Ebana samahani kidogo, unaweza kuniruhusu nipokee simu ya Mzee Kilomoni naona ananipigia hapa muda mrefu?

LUQMAN: Unataka kunificha anachotaka kukwambia Kilomoni? Tumefikia huko kweli Levy?

LEVY: Sasa nakuheshimu kwa kuomba uruhusu nipokee simu yake unaanza lawama. Tangu asubuhi ananipigia ujue.. Mi nakausha sipokei.

LUQMAN: Si upokee uweke laudispika na mimi nisikie? Unataka kuninyima nini wewe mdogo wake Mkwabi?

LEVY: Sasa ndo tatizo lenu vijana wa kizazi cha Kikwete. Yaani niongee kwa laudispika na mtoto wa mjini kama Mzee Kilomoni? Naona kiburi cha MO kimewajaa mpaka ninyi wafuasi wake.

LUQMAN: Isiwe tabu. Ongea naye halafu unitonye alichosema. Inawezekana anakuomba ushauri wa namna ya kutumia hati za mali za Simba kuchukulia mkopo kwa naniii.

LEVY: Bora nisiongee naye kuliko kukueleza alichoniambia. Ngoja... Imeingia meseji yake hapa... Anasemaaa... “Kijana naona umebanwa sana leo, nimepiga simu tangu alfajiri hupokei. Anyway hata mimi sijapokea simu ya naniiii wiki ya pili sasa anapiga kila siku. Sitaki hata kusikia sauti yake yule kijana anayetaka kutuingiza mjini kwa magirini ya mikataba mfu isiyoeleweka kama minyoo ya Rufiji.”

LUQMAN: Hiyo ni meseji ya kutunga, Kilomoni hawezi kuacha kupokea simu ya kijana wake. Wewe utakuwa umechanganya watu, mzee Akilimali unahisi ndio Kilomoni.

LEVY: Utambue tu kuwa Rais wa TFF ya Misri kampiga chini kocha wao, kisha akajipiga chini mwenyewe. Baada ya hapo wajumbe wote wa kamati zilizohusika na timu mwenyeji kutolewa na Wangoni wa Sauzi. Hiyo ndo dhana ya kuwajibika. Sisi tumemuacha Amunike peke yake ndo asepe na ‘sendozi’ zake. Kina tifutifu wameendelea kukalia viti.

LUQMAN: Hata Misri hajajiuzulu kila mtu. Mbona wachezaji hawajajiuzulu? Sijasikia mashabiki wamejiuzulu. Hapa ni kutoana kafara tu, tumemtosa Amunike imetosha. Sijui Taifa Stars tumpe Kashasha?

LEVY: Achana na wachezaji. Hata waandishi na watangazaji wa michezo wangejiuzulu waanze kutangaza vipindi vya salamu na kuandika habari za ufugaji wa nyuki. Maana Stars ya magazetini na redioni hata akija Messi hapati namba.

LUQMAN: Ulikwenda kwenye pati la besidei ya Tanasha wa Diamond na Mama Dangote Mlimani City?

LEVY: Kaka tutafute pesa aiseee.... Kile kitoto kimegawa ndinga za mamilioni kwa Bi. Mkubwa wake na mkewe ‘nyu modeli’ kama vile kinagawa vocha za jero jero. Kijamaa kina pesa kile tuache kuvunga aiseee. Hivi zile gari za kweli au za maboksi? Ujue zile ni ‘vieiti’ kaka siyo IST?

LUQMAN: Hela zinaleta ujana, zinachubua ngozi, zinaleta uhendsam na ubyutifu. Kuna kipindi nilikuwa nikiwaangalia Mama Diamond na Tanasha, nikashindwa kung’amua nani mkubwa. Ilibidi niumize kichwa, nikatumia hadi fo-figa.

LEVY: Kwa kasi hii. Mpaka mwakani Mama Dangote atakuwa mdogo kiumri kuliko Wema, Uwoya, Mobeto, Lulu na Nandy. Kifupi atajikuta anamwamkia shikamoo Zari na kumsalimia Mwambo vipi Tiffah. Kweli pesa inahamisha milima mabonde na mito.

LUQMAN: Hasa hasa ukimwangalia mama Dangote anaweza kuwa na umri wa miaka mingapi?

LEVY: Yule anaweza kuwa mdogo wake wa tano na Sugu... Yaani Sugu au Dudubaya ni wakubwa kwa Mama Dangote.

LUQMAN: Lakini, Mama Dangote anaweza kuwa amevuka miaka 40, si eti Levy?

LEVY: Unalazimisha kupewa kesi ya kughushi. Uwe unaangalia sura za kuvuka miaka 40. Hivi huoni hata tabia zake ni za chini ya miaka 40? Angekuwa Chadema au CCM bila shaka alifaa kuwa Bavicha au UVCCM. Na bado angeonekana kijana zaidi ya kina Jokate na Halima Mdee.

LUQMAN: Nakumbuka mwaka 2010 siku ile Diamond Jubilee mtoto wake alipobeba tuzo tatu Kili Music Awards, nilikutana naye nikamwamkia, ila sasa hivi nahisi tukionana nitamfosi aniamkie yeye, maana nazeeka yeye anakuwa binti.

LEVY: Ndiye mkwe mwenye umri na umbile dogo kuliko wakweze. Ila nina shaka Tanasha anatumia ndumba yule dem. Simba toka mbuga ya Tandale kawa mwepesi sana kwake. Zari alisubiri alete watoto wawili duniani ndipo aambulie ule mjengo wa Sauz. Wema alisota miaka saba ndipo akapata Morano ya kuungaunga siku ya besidei. Nadhani ndo maana alisusa na kuizuia mbali huko. Huyu Tanasha hata mwaka haujaisha tayari ana ‘vieiti’.

LUQMAN: Sasa uchawi wa Tanasha nini? Ile rangi yake? Kasura kake? Huwezi labda yaliyomo yamo, si unaona hata Ali Kiba alimuimbia anagharamia, Christian Bella akaishia kutoa macho?

LEVY: Tanasha hana shepu bomba kama ya Wema wala sura tamu kama ya Zari. Hana kimo amazing kama cha Mobeto wala pozi na lips mzuka kama za yule Disii. Hakuna zaidi ya ndumba. Maana kama Kiingereza hamfikii Wema. Dogo karogwa yule sema atakuja kushituka kumepambazuka. Uchawi wa vile kule Vietnam unaitwa vivie so phritey... kwa Lugha ya Kimara, Mwananyamala na Mabibo maana yake ni Pakua Pausha mpaka Bandama. Dogo atapaushwa kama kaogeshwa kwa JIKI.

LUQMAN: Swali la mwisho Levy; Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron ni bwana mdogo sana kwa mkewe, Brigitte. Kimbembe ni kuwa Brigitte ana watoto wakubwa kuliko Macron. Yaani, Rais Macron anaitwa dogo na watoto wake. Umesema Mama Dangote anazidiwa umri na wakwe zake, yaani wanawake wa kijana wake Platnumz. Hii imekaaje? Inyooshe.

LEVY: Sababu ya Diamond kumwagana na Zari ni maumbile ya watoto wake. Ilifika wakati watoto walikuwa wanamtazama Diamond kama ‘koini’ sakafuni? Marefu na mbavu pana kama ‘Mwarabu Faita’. Sasa Simba wa Tandale akaona kuna siku atavunjwa mbavu kwa kipigo kama atamzingua Zari mbele yao. Wafuatilie wale madogo wanakua kila siku kama miashoki. Amini nakuambia Zari ni mkubwa kwa Mama Dangote. Ukitaka kuamini Mama Dangote mdogo, mtazame mumewe, umbile na umri pamoja na pozi zake kama Ommy Dimpoz.