Tuzo za mchezaji, kocha bora mambo safi TFF

Muktasari:

Alisema watakuwa wakitoa million moja kwa kila mchezaji na kocha atakayeibuka bora kila ndani ya mwezi husika na kuweka wazi kuwa lengo la kufanyaivyo ni kuongeza chachu ya ushindani.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesaini mkataba wa million 17 na Bikosports kwa ajili ya udhamini wa tuzo ya mchezaji bora na kocha bora wa mwezi.
Akizungumza Dae es Salaam, Jana Msemaji wa Bikosports, Jeff Lea alisema udhamini huo umeanza mwezi Desemba hadi mwisho wa msimu huu.
Alisema watakuwa wakitoa million moja kwa kila mchezaji na kocha atakayeibuka bora kila ndani ya mwezi husika na kuweka wazi kuwa lengo la kufanyaivyo ni kuongeza chachu ya ushindani.
"Huu ni mwanzo tu kwa Bikosports kushirikiana na TFF pamoja na Bodi ya Ligi hivyo nazani mambo mazuri zaidi yataendelea kulingana na ushirikiano mzuri baina yetu na wao," alisema.
Lea aliongeza kuwa mbali na fedha watakayokuwa wakitoa kila mwezi pia wanampango wa kuambatanisha na kombe dogo ambalo litakuwa na majina ya washindi na mwezi husika lengo likiwa ni kama kumbukumbu kwa washindi tofauti na fedha ambazo zinatumika.